LIVE STREAM ADS

Header Ads

Msaada wa maibabu unahitajika

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Mkazi wa Kijiji cha Milola, Kata ya Milola mkoani Lindi, Esha Selemani Peleu.


Na Dotto Mwaibale, Lindi
Mkazi wa Kijiji cha Milola kilichopo Kata ya Milola mkoani Lindi, Esha Selemani Peleu }35 } maisha yake yapo hatarini kutokana na moyo wake kuwa na tundu na ameshindwa kupata matibabu kwa sababu hana fedha.

Akizungumza na waandishi wa habari, Esha amesema alianza kuwa na changamoto ya maradhi hayo mwaka 2020 ambapo alikwenda Hospitali ya Misheni ya Ndanda na baada ya kufanyiwa vipimo moyo wake uligundulika kuwa na tundu.

Amesema daktari aliyemuhudumia alimuandikia dawa ambazo hazikumbuki kwani vyeti vyake vilipotea lakini vilikuwa ni vidonge vidogo vyeupe ambavyo alielekezwa avikate mara nne na avitumie kutwa mara moja na kuwa gharama ya vipimo na hizo dawa ilikuwa ni zaidi ya Sh.60,000.

Amesema fedha hizo alipewa na mume wake ambaye ametengana naye baada ya kupata changamoto hiyo na kuwa sasa anaishi na mtoto wake kwa wazazi wake ambao hawana uwezo na tangu apate matibabu hayo huu ni mwaka wa tatu anaishi kwa mateso na hana raha ya maisha kutokana na maumivu makali anayoyapata.

''Naishi kwa mashaka kifua kinabana, napumua kwa shida nikienda kuchota maji napata maumivu makali wakati wa kupumua nalazimika kuvuta pumzi kidogokidogo ndipo napata nafuu haya ndiyo maisha yangu ya kila siku na siwezi kukaa tu nyumbani pasipo kufanya kazi naomba msaada wenu mwenzenu nakuja jameni'' amesema Esha.

Amesema changamoto hiyo ilimuanza wakati anajiandaa kulala alipata mshituko wa moyo na akapoteza kumbukumbu tangu wakati huo mwili wake umekuwa ukidhohofu na kumfanya asijue cha kufanya hivyo anamuomba Waziri wa Afya Ummy Mwalimu na wadau wengine mbalimbali wamsaidie kupata matibabu kwani wakati mwingine hata kula yake na mwanaye huyo aliyemtaja kwa jina moja la Rumaydha imekuwa ya changamoto kutokana na mazingira anayoishi ya kutokuwa na fedha ya kujikimu.

Taasisi na mtu yeyote ambaye ataguswa kumsaidia dada yetu huyu ambaye anapitia katika wakati mgumu kutokana na maradhi hayo yanayomsumbua na kushindwa kufanya kazi yoyote ambayo inaweza kumpatia kipato na kupata matibabu anaweza kuwasiliana naye moja kwa moja kwa namba ya simu 0785 192412 au namba 0754362990 na Mungu atakubariki kwani kutoa sio mpaka uwe na fedha nyingi hata hiyo Shilingi 2,000 yako kwake itamtosha.

No comments:

Powered by Blogger.