Mwenge wa Uhuru 2023 waridhishwa na miradi wilayani Ikungi
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Mkuu wa Wilaya ya Singida, Mhandisi Paskas Muragili (kulia), akimkabidhi Mwenge wa Uhuru, Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Thomas Apson baada ya kumaliza mbio za kukagua miradi katika wilaya hiyo, Septemba 25, 2023.
Na Dotto Mwaibale, Ikungi
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa 2023, Abdalla Shaib Kaim ameridhishwa na utekelezaji wa miradi yote illyopitiwa na kukaguliwa na Mwenge huo wilayani Ikungi mkoani Singida na kueleza kuwa imekamilishwa kwa viwango vya ubora wa hali ya juu ambao umeendana na thamani ya fedha.
Kaim akizungumza na wananchi wa wilaya hiyo Septemba 26, 2023 ikiwa ni siku yake ya nne ya mbio za mwenge amesema miradi yote ipo vizuri na kuwa mapungufu madogo madogo yaliyopo aliomba yafanyiwe kazi haraka ili kuiboresha zaidi.
Kiongozi huyo ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi kwa kubuni chanzo kipya cha mapato ambacho ni stendi mpya ya mabasi iliyojengwa eneo la Unyahati kutokana na fedha za mapato ya ndani.
“Niwapongeze kwa ubunifu mkubwa mlioufanya kwa kuanzisha stendi hii ambayo itakuwa chanzo kikubwa cha mapato” amesema Kaim.
Aidha, ameagiza uongozi wa halmashauri hiyo kujenga vizimba kwa ajili ya kuwekea taka pamoja na kupanda miti kuzunguka stendi hiyo ili iwe katika mandhari nzuri.
Kaim amesema Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan imekuwa ikileta fedha nyingi kwenye halmashauri kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali hivyo ni jukumu la watendaji kuhakikisha wanaisimamia ili iwe inajengwa kwa viwango vya ubora ambavyo vinaendana na thamani ya fedha.
Awali Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Thomas Apson akitoa taarifa ya miradi iliyotembelewa na kukaguliwa na Mwenge wa Uhuru amesema ni saba na ina thamani ya Sh.Bilioni 2.14 na program mbalimbali tano.
Ametaja baadhi ya miradi iliyotembelewa kuwa ni mradi wa maji uliopo Kijiji cha Matare Kata ya Unyahati ambao umegharamiwa na fedha za Benki ya Dunia kupitia programu ya pforR uliotengewa Sh.386,898,900 na mradi wa ujenzi wa vyumba vinne vya madarasa na matundu sita ya vyoo uliopo Shule ya Msingi ya Matare katika Kijiji cha Matare Kata ya Unyahati.
Ametaja miradi mingine kuwa ni Kitalu cha miti uliopo Kijiji cha Mungaa Kata ya Mungaa ambao tangu kuanzishwa kwake jumla ya miche 965,000 imezalishwa na kuwa unatekelezwa na Shirika lisilo la Kiserikali la Anti-Desert- Environment Scheme (ADESE) kwa kushirikiana na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzani (TFS) na unafadhiliwa na Shirika lisilo la Kiserikali la Trees for the Future lililopo mjini Singida.
Apson ametaja miradi mingine kuwa ni Kikundi cha kufyatua matofali Vijana Chapakazi Ikungi ambacho kilianzishwa Desemba 6, 2022 na kukopeshwa mkopo wa Sh.Milioni 25 na Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi na ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Ikungi.
Ametaja programu zilizotembelewa na Mwenge huo kuwa ni ya mapambano dhidi ya Malaria na mapambano dhidi ya dawa za kulevya, damu salama, mapambano ya VVU, masuala ya lishe, mapambano dhidi ya rushwa na Ukimwi na usafi wa mazingira.
Apson amesema Mwenge huo umekimbizwa umbali wa kilometa 137.7.ukifanya shughuli za uwekaji wa jiwe la msingi, uzinduzi na kutembelea miradi hiyo saba na kuwa kauli mbiu ya mbio hizo za Mwenge wa Uhuru 2023 ni Tunza Mazingira, Okoa Vyanzo vya maji kwa Ustawi wa Viumbe Hai na Uchumi.
Mbunge wa Viti Maalumu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)_Nusrat Hanje amepongeza kazi kubwa inayofanywa na Rais Samia kwa kutoa fedha nyingi kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.
“Kwa dhati kabisa ya moyo wangu niipongeze Serikali ya Rais Dk. Samia kwa kutuwezesha sisi watu wa Mkoa wa Singida na nimpongeze kaka yangu Mbunge Miraji Mtaturu kwa kusimamia vizuri miradi inayoletwa na kuhakikisha inakamilika kwa thamani ya fedha zilizotolewa” amesema Hanje.
Akitoa salamu Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Singida, Aysharose Mattembe naye ameungana na viongozi wenzake akiwepo Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ikungi, Mika Likapakapa kumshukuru Rais Samia kwa kazi kubwa anayoifanya na kutoa fedha nyingi za kutekeleza miradi ambapo aliwaomba wananchi ilipo miradi hiyo kutunza miundombinu yake.
Kesho Septemba 27 timu nzima ya wakimbiza Mwenge huo wakiongozwa na Kiongozi wao wa Kitaifa wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2023, Abdalla Shaib Kaim watatembea na kukagua miradi mbalimbali katika Halmashauri ya Itigi.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Thomas Apson akimkabidhi Risala ya Utii Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2023, Abdalla Shaib Kaim ili akamkabidhi Rais Samia Suluhu Hassan.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Ikungi, Rashid Rashid akiwa ameushika mwenge huo kabla ya kuanza kukimbizwa wilayani humo.
Vijana wa Skauti Khalid Abdallah (kushoto) na Mafongwe Tenga wakimvika Skafu Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2023 wakati wakimkarisha Iilaya ya Ikungi kuanza kukimbiza mwenge huo.
Vijana wa Skauti wakimvika Skafu Mkimbiza mbio za Mwenge wa Uhuru, Atupokigwe Elia kutoka Dodoma wakati wakimkarisha Iilaya ya Ikungi kuanza kukimbiza mwenge huo
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2023, Abdalla Shaib Kaim, akipanda mche wa mparachichi katika viwanja vya Shule ya Msingi Matare ikiwa ni kuhifadhi mazingira.
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2023, Abdalla Shaib Kaim akipata maelezo kutoka kwa Mtaalam wa masuala ya Lishe wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi.
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2023, Abdalla Shaib Kaim, akionesha umahiri wa kupika mboga za majani alipotembelea banda la Lishe katika Shule ya Msingi Matare.
Vijana wa Skauti wakiwa tayari kwa mapokezi ya wakimbiza Mwenge wa uhuru 2023 eneo la Njiapanda barabara ya Arusha na Makiungu.
Vijana wa hamasa wakionesha umahiri wa kucheza sarakasi wakati wa mapokezi hayo.
Vijana wa Skauti wakionesha ukakamavu.
Vijana wa Skauti wakiwa kwenye mapokezi hayo.
Wajumbe wa kamati ya ulinzi na Usalama Wilaya ya Ikunghi. wakionesha ukakamavu wakati wa mapokezi hayo.
Wakimbiza mwenge wa Uhuru 2023 Wilaya ya Ikungi wakiwa tayari kwa kazi hiyo. Kutoka kushoto ni Ibrahim Njoka, Patrick Mande, Lucia Silvester, Paskali Charles, Jacob Mgwama na Rebeca Julius.
Shamrashamra za mapokezi hayo zikiendelea.
Viongozi wa Wilaya ya Ikungi wakionesha furaha zao wakati wa mapokezi wa mwenge huo.
Viongozi wa Wilaya ya Ikungi na Manispaa ya Singida wakifurahi pamoja wakati wa mapokezi hayo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Singida, Jeshi Lupembe akionesha furaha yake wakati wa mapokezi hayo.
Mstahiki Meya wa wa Manispaa ya Singida, Yagi Kiaratu naye akionesha furaha yake wakati wa mapokezi hayo.
Mbunge wa Viti Maalum wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Nusrat Hanje akimshukuru Rais Samia kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuwaletea maendeleo wana Singida na Taifa kwa ujumla.
Wakimbiza Mwenge wa Uhuru 2023 wakiwa tayari kupokelewa Wilaya ya Ikungi baada ya kumaliza mbio zao Manispaa ya Singida.
Mkufunzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2023, Meja Musa Ngomambo, akizungumza wakati akiwaaga wananchi wa Manispaa ya Singida tayari kwa kukimbiza mwenge huo Wilaya ya Ikungi.
Viongozi wa Wilaya ya Ikungi wakionesha tabasamu wakati wa kupokea mwenge huo. Kutoka kushoto ni Katibu Tawala wa wilaya hiyo, Rashid Rashid, Mkuu wa Polisi Mrakibu wa Polisi (OCD)_ Suzana Kidiku.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Abdalla Shaib Kaim, akizungumza wakati akiwaaga viongozi wa Manispaa ya Singida.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Thomas Apson, akimkabidhi mafuta ya alizeti Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Abdalla Shaib Kaim.
Umati wa watu ukiwa katika mapokezi ya Mwenge wa Uhuru eneo la Njia Panda
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Makiungu wakiwa katika mapokezi ya Mwenge wakati wa ukaguzi wa mradi wa kitalu cha miti .uliopo Kijiji cha Mungaa Kata ya Mungaa.
Muonekano wa kitalu hicho cha miti.
Mkimbiza Mwenge wa Uhuru 2023, Emmanuel Hondi kutoka Babati Mkoa wa Manyara, akikabidhiwa taarifa ya mradi wa kitalu hicho cha miti.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mungaa wakati katika mapokezi ya mwenge huo.
Mapokezi ya mwenge huo yakiendelea.
Taswira ya mapokezi ya Mwenge huo Puma ambapo ulitembea na kukagua programu mbalimbali.
Mratibu wa Programu ya Malaria Wilaya ya Ikungi, Isaya Mawazo akitoa taarifa ya mapambano dhini ya malaria. kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2023, Abdalla Shaib Kaim.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2023, Abdalla Shaib Kaim.akigawa vyandarua vilivyotolewa na Bohari ya Dawa (MSD) kwa ajili ya mapambano dhidi ya malaria.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2023, Abdalla Shaib Kaim. akipata maelezo ya mapambano dhidi ya vitendo vya rushwa alipotembea banda la Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU) willayani humo._
Mashujaa wa Shujaa wa Maendeleo na Ustawi wa Jamii Tanzania (SMAUJATA)_ wakiongozwa na Mwenyekiti wao Mkoa, Shujaa Dismas Kombe nao walikuwepo kwenye mapokezi ya Mwenge wa Uhuru 2023 eneo la Puma.
Madiwani na viongozi mbalimbali wakiwa kwenye mapokezi ya mwenge huo Stendi ya zamani ya mabasi ya wilaya hiyo ambapo mkesha wa mwenge ulifanyika. Wa pili waliokaa mbele kutoka kushoto ni Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi, Abubakar Muna.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2023, Abdalla Shaib Kaim.akipata maelezo ya mapambano ya kudhibiti dawa za kulenya.
Programu ya usafi na utunzaji wa mazingira ikifanyika.
Vijana wa Kikundi cha kufyatua matofali Vijana Chapakazi Ikungi wakiwa katika mapokezi ya mwenge huo wakati ulipofika kukagua kikundi hicho.
Mwenyekiti wa kikundi hicho, Mwanahamisi Omari (Aliyevaa kofia)_ akijibu kwa ufasaha maswali aliyokuwa akiulizwa na kiongozi wa mbio za mwenge baada ya kumsomea taarifa ya mradi huo.
Askari wa Jeshi la Akiba wakihimarisha ulinzi wakati Mwenge wa Uhuru 2023 ulipowasili Stendi ya Mabasi ya zamani ya wilaya hiyo ambapo ulikesha.
Wakimba mwenge wa uhuru wakipitia nyaraka mbalimbali za ujenzi wa Stendi mpya ya Mabasi ya Wilaya ya Ikungi.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ikungi, Mika Likapakapa akitoa salamu za chama wakati wa mapokezi hayo. Kulia ni Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki Miraji Mtaturu.
Chifu Thomas Mgonto (kulia( kutoka Siuyu wilayani humo akizungumza na Vijana kuhusu kuzingatia maadili.
Uwekaji wa jiwe la msingi la Stendi Mpya ya Mabasi Wilaya ya Ikungi ukifanyika.
Meneja wa Ruwasa Wilaya ya Ikungi Mhandisi Hope Lihundi akitoa maelezo ya mradi wa maji wa Kata ya Matare kwa Kiongozi wa mbio za mwenge kabla hajauzindua mradi huo.
Kiongozi wa mbio za mwenge Abdalla Shaib Kaim akimuhoji Mhandisi wakati akikagua miundombinu ya ujenzi wa Shule ya Msingi Matare.
Ukaguzi wa madawati na meza zake ukifanyika katika shule hiyo
Muonekano wa moja ya darasa lililojengwa kwenye shule hiyo.
No comments: