LIVE STREAM ADS

Header Ads

Kiwanda kipya cha vifungashio chatambulishwa Shinyanga

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Mkurugenzi wa kiwanda kidogo cha kutengeneza vifungashio cha AZAT, Azza Hilal Hamad akionesha aina za vifungashio vinavyotengenezwa kwenye kiwanda hicho kilichopo mjini Shinyanga.
Na Kadama Malunde, Malunde 1 Blog
Mkurugenzi wa kiwanda kidogo cha kutengeneza vifungashio cha AZAT, Azza Hilal Hamad akionyesha vifungashio vinavyotengenezwa na kiwanda hicho.
Mkurugenzi wa kiwanda kidogo cha kutengeneza vifungashio cha AZAT, Azza Hilal Hamad ametambulisha rasmi kiwanda hicho pamoja na vifungashio vinavyotengenezwa kwenye kiwanda hicho kilichopo Nhelegani katika Manispaa ya Shinyanga mkoani Shinyanga.

Azza ametambulisha kiwanda cha AZAT na bidhaa hizo Jumatano Oktoba 18, 2023 wakati akisherehekea siku yake ya kuzaliwa ‘Birthday’.

Ametumia fursa hiyo kuwakaribisha wadau kununua vifungashio hivyo ambavyo tayari vipo sokoni ili kukabiliana na changamoto ya uhaba wa vifungashio pamoja na kutunza mazingira.

“Katika kiwanda hiki cha AZAT tunatengeneza vifunganishio rafiki kwa mazingira kwa kutumia karatasi ngumu na bora. Kwa sasa tuna vifungashio aina tano na tunatengeneza kulingana na mahitaji ya mteja, kuanzia robo kilo hadi kilo tano. Vifungashio hivi havilowani haraka. Hata ukihitaji nembo ya Biashara yako tuiweke, tunakuwekea kwenye vifungashio” ameeleza Azza.

“Tunawakaribisha sana wadau wetu wakiwemo wafanyabiashara , wajasiriamali na wananchi wote. Vifungashio hivi ni bora na vigumu, vinafaa kutumika kufungia bidhaa kwenye maduka ya dawa za binadamu, dawa za mifugo, Super Market, wauza chips, mama lishe, wauza matunda, Hotelini n.k” ameongeza.

Amesema kwa yeyote anayehitaji vifungashio vya AZAT bidhaa tayari zipo kwenye maeneo mbalimbali au afike kwenye kiwanda cha AZAT kilichopo Nhelegani Mjini Shinyanga au apige simu namba 0787653394
Mkurugenzi wa kiwanda kidogo cha kutengeneza vifungashio cha AZAT, Azza Hilal Hamad akionyesha vifungashio vinavyotengenezwa na kiwanda hicho.
Mkurugenzi wa kiwanda kidogo cha kutengeneza vifungashio cha AZAT, Azza Hilal Hamad akionyesha vifungashio vinavyotengenezwa na kiwanda hicho.
Mkurugenzi wa kiwanda kidogo cha kutengeneza vifungashio cha AZAT, Azza Hilal Hamad akionyesha vifungashio vinavyotengenezwa na kiwanda hicho.
Mkurugenzi wa kiwanda kidogo cha kutengeneza vifungashio cha AZAT, Azza Hilal Hamad akionyesha vifungashio vinavyotengenezwa na kiwanda hicho.
Mwonekano wa vifungashio.
Mwonekano wa vifungashio.

No comments:

Powered by Blogger.