LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mtoto amuua baba yake kwa kumkata mapanga

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) Pili Mande

Na Said Hauni, Lindi
Mkulima wa Kijiji na Kata ya Namapwia, Wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi, Musa Michenje (60) amefariki dunia baada ya kukatwa mapanga na mtoto wa kaka yake aitwae Nkono Malenga (35) kutokana na ugomvi wa kugombania mti wa mkorosho.

Taarifa kutoka kijijini humo ambazo zime thibitishwa na uongozi wa Kata na Jeshi la Polisi inaeleza mauwaji hayo yamefanyika Oktoba 04, 2023 saa 11:00 alasiri.

Mashuhuda wa tukio hilo akiwemo Diwani wa Kata hiyo, Omari Lingumbende wameeleza Michenje na Malenga ni mtu na mwanawe, walikuwa wakigombea mkorosho uliokuwa kwenye mpaka wa shamba kati ya marehemu na kaka yake Malenga.

Mashuhuda hao Yusufu Ismaili, David Michael wamesema kutokana na mkorosho huo kuwa mpakani kaka mtu Malenga aliamua kumuachia mdogo wake Michenje.

Wamesema siku hiyo Michenga akiwa anaokota korosho kwenye mkorosho huo,mtoto wa kaka yake aitwse Nkono alifika na kumtaka aache kuokota.

Walisema kutokana na mabishano yaliyokuwa yamejitokeza mtoto huyo aliyekuwa na panga mkononi alianza kumshambulia baba yake huyo mdogo kwa kumkata maeneo mbalimbali ya mwili wake na kusababisha kifo hapo hapo.

Diwani wa Kata ya Namapwia, Omari Liungimbende amekiri kutokea kwa mauwaji hayo na kueleza tayari mtuhumiwa amekamatwa na kukabidhiwa Jeshi la Polisi kuendelea na taratibu zingine za kishetia.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, Pili Mande amekiri kushikiliwa kwa mtuhumiwa huyo na kueleza atafikishwa mahakamani baada ya kukamilishwa upelelezi.

No comments:

Powered by Blogger.