LIVE STREAM ADS

Header Ads

Waziri Mhagama atembelea Banda la NSSF Katika Maonesho ya Wiki ya Vijana

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu- Jenista Mhagama ametembelea banda la NSSF wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Vijana mkoani Manyara ambapo amezindua Wiki hiyo kwa niaba ya Waziri Mkuu- Kassim Majaliwa.

Naye Meneja wa Sekta isiyo rasmi, Rehema Chuma amemueleza Waziri Mhagama kuwa “NSSF imeendelea kupanua wigo kwa kuwafikia vijana wanaosoma katika vyuo vya elimu ya juu ili wajiunge na kuchangia kwa maisha yao ya sasa na ya baadaye, mwitikio wa wanaojiunga ni mkubwa, ambapo katika vyuo vya elimu ya juu tumeweza kufikia vyuo vinane na tayari wanavyuo 1,050 wameshajiunga na mpango wa kujichangia kwa hiari”.

NSSF inashiriki maonesho hayo yanayofanyika katika uwanja wa stendi ya zamani Babati mkoani Manyara kwa ajili ya kutoa elimu ya hifadhi ya jamii, kusajili wanachama wapya kutoka sekta binafsi na sekta isiyo rasmi, elimu kuhusu huduma za NSSF kidijitali, elimu kuhusu mapambano dhidi ya rushwa, uwekezaji unaofanywa na NSSF.

No comments:

Powered by Blogger.