LIVE STREAM ADS

Header Ads

Taasisi ya InfoNile yatambulisha jukwaa la NileWell

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Taasisi ya Waandishi wa Habari ya InfoNile yenye makao yake makuu nchini Uganda imetambulisha jukwaa la NileWell lenye lengo la kuwaleta pamoja waandishi wa habari na wataalam mbalimbali ili kufanya kazi pamoja.

Kwa Tanzania, warsha ya kutambulisha jukwaa hilo imefanyika Ijumaa Novemba 24, 2023 katika ofisi za shirika la mazingira na maendeleo (EMED zilizopo jijini Mwanza.

Akizungumza wakati wa warsha hiyo, Mratibu wa InfoNile nchini Tanzania, Said Sindo amesema jukwaa hilo litakuwa chanzo muhimu cha upatikanaji wa tafiti na takwimu mbalimbali za kisayansi ambazo zitawasaifia waandishi wa habari katika majukumu yao.

Mhadhiri Msaidizi Chuo Kikuu SAUT ambaye pia ni Mtafiti, Ngogo Mang'enyi amesema awali kulikuwa na ushirikiano duni baina ya watafiti na waandishi wa habari hivyo jukwaa hilo litaondoa Mwanza huo.

Baadhi ya washiriki katika warsha hiyo akiwemo Tonny Alphonce na Esther Baraka wameipongeza taasisi ya InfoNile kwa kuja na jukwaa la NileWell ambalo litakuwa chanzo cha kuaminika kwa waandishi wa habari kupata tafiti mbalimbali.
Na George Binagi- GB Pazzo, BMG
Mratibu wa taasisi ya InfoNile nchini Tanzania, Said Sindo akizungumza kwenye warsha ya kutambulisha jukwaa la NileWell kwa wadau mbalimbali wakiwemo waandishi wa habari na wanamazingira jijini Mwanza.
Mratibu wa taasisi ya InfoNile nchini Tanzania, Said Sindo akizungumza kwenye warsha ya kutambulisha jukwaa la NileWell.
 Mratibu wa taasisi ya InfoNile nchini Tanzania, Said Sindo akizungumza kwenye warsha ya kutambulisha jukwaa la NileWell.
Afisa Miradi Shirika la EMEDO, Urther Mgema (kushoto) akizungumza wakati wa warsha hiyo. Kulia ni Mratibu wa taasisi hiyo nchini Tanzania, Said Sindo.
Afisa Uchechemuzi shirika la EMEDO, Mary Francis akizungumza wakati wa warsha hiyo.
Baadhi ya waandishi wa habari jijini Mwanza wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mratibu wa InfoNile nchini Tanzania, Said Sido (wa tatu kulia).
Washiriki wa warsha hiyo wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mratibu wa Taasisi ya InfoNile nchini Tanzania, Said Sindo (wa kwanza kulia).
PIA SOMA>>> HABARI ZAIDI HAPA

No comments:

Powered by Blogger.