LIVE STREAM ADS

Header Ads

Rais Mstaafu Kikwete afanya mazungumzo na Rais Ruto

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Rais Mstaafu was Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Kenya, William Samoei Ruto tarehe 19 Novemba, 2023 Ikulu jijini Nairobi.

Rais Mstaafu Kikwete ambaye ni Mlezi wa Jukwaa la Vijana wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (YouLead Summit) pamoja na mambo mengine, amefika Ikulu ya Nairobi kumjulisha Rais Ruto kuhusu masuala mbalimbali ya Mkutano wa Jukwaa hilo unaotarajiwa kuanza Novemba 20, 2023 jijini Nairobi.

No comments:

Powered by Blogger.