Kituo cha mafunzo ya kilimo kilichoanzishwa na Barrick chaendelea kunufaisha wakulima wilayani Kahama
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Wakulima wakipokea mkopo wa pembejeo za kilimo kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mboni Mhita, zilizotolewa na Halmashauri ya Wilaya ya Kahama kwa kushirikiana na Barrick.
Mkuu wa wilaya ya Kahama, Mboni Mhita, akiongea na wananchi wakati wa hafla ya kukabidhi mkopo wa pembejeo kwa wakulima uliotolewa na Manispaa ya Wilaya ya Kilimo kwa kushirikiana na Barrick.
Mkuu wa wilaya ya Kahama,Mboni Mhita, akihakiki pembejeo za kilimo zilizotolewa na Manispaa ya Kahama kwa kushirikiana na Barrick.
Wakulima wakipokea mkopo wa pembejeo za kilimo kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mboni Mhita, zilizotolewa na Halmashauri ya Wilaya ya Kahama kwa kushirikiana na Barrick
Wakulima wakipokea mkopo wa pembejeo za kilimo kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mboni Mhita, zilizotolewa na Halmashauri ya Wilaya ya Kahama kwa kushirikiana na Barrick
Wakulima wakipokea mkopo wa pembejeo za kilimo kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mboni Mhita, zilizotolewa na Halmashauri ya Wilaya ya Kahama kwa kushirikiana na Barrick
Wakulima waliopatiwa mkopo wa pembejeo wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mboni Mhita.
****
Kituo cha Rasilimali cha kilimo Mwendakulima kilichopo wilayani Kahama mkoani Shinyanga, kilichoanzishwa na Mgodi wa Barrick Buzwagi kwa ajili ya kuwafanya wakazi wa vijiji vilivyopo jirani na mgodi huo kinaendelea kuwanufaisha Wakulima ambapo hadi kimetoa mafunzo kwa wakulima 4,200
Lengo la kuanzishwa kituo hiki lilikuwa ni kuhakikisha wakulima wanakuwa na maisha bora endelevu kupitia kilimo baada ya kufungwa uzalishaji katika mgodi huo mwaka 2018 ambapo kwa sasa kinazidi kuleta mafanikio kwa wakulima kuongeza uzalishaji wa mazao kutokana na kuwezeshwa kwa kupatiwa mafunzo ya kuendesha kilimo bora na ufugaji na kupatiwa mikopo ya pembejeo na madawa ya kilimo.
Hayo yamebainishwa wakati wa hafla ya Halmashauri ya Manispaa ya Kahama kwa kushirikiana na Barrick Buzwagi kutoa mkopo wa pembejeo za kilimo kwa wakulima wapatao 90 waliohitimu mafunzo katika kituo hicho kwa ajili ya kuongeza tija katika shughuli zao. Mgeni rasmi katika hafla hiyo alikuwa ni Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mboni Mhita ambaye aliwataka wakulima kuzingatia marejesho ya mkopo huo ili kufanya programu ya mpango huu kuwa endelevu na kuendelea kunufaisha wakulima wengi zaidi.
“Kumekuwepo na desturi ya baadhi ya wakulima kupewa mikopo na kutokomea bila marejesho hali ambayo inasababisha miradi ya ukopeshwaji kukwama, sasa nawakata wakulima mliopatiwa pembejeo hizo leo mkazingatie marejesho ili wengine nao wanufaike pia naipongeza Barrick kwa kujenga kituo hiki kinatachoendelea kunufaisha wananchi kwa kipindi kirefu hata baada ya kufunga shughuli zao kabisa”, alisema Mhita.
Mkuu wa Idara ya kilimo wa Manipaa hiyo ambayo inasimamia shughuli za uendeshaji wa kituo hicho, Jeremia Inegeja, alisema pembejeo walizopatiwa wakulima ni pamoja na mbolea ya ruzuku, mbegu za mazao za mahindi, mpunga na alizeti na viuatilifu vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya shilingi milioni 70 zitakazotumika kwenye jumla ya ekari 300 za wakulima wa kata za Mondo na Mwendakulima msimu huu 2023/24.
Alisema mradi huo wa kuwawezesha wakulima tangu uanzishwe umesaidia kuongeza uzalishaji mazao kwa wakulima ikilanginishwa na kabla ya matumizi ya pembejeo. “Kabla ya wakulima kupatiwa pembejeo hali ya uzalishaji zao la mahindi ilikuwa ni gunia tano kwa ekari moja, lakini baada ya kutumia pembejeo uzalishaji umeongezeka na kufikia gunia 25 kwa ekari moja”,alisema Inegeja .
Kwa upande wa uzalishaji wa zao la mpunga uzalishaji umeongezeka kutoka gunia 12 kwa ekari hadi gunia 30 huku alizeti uzalishaji pia ukiongezeka kutoka gunia sita za awali hadi gunia 12 baada ya matumizi ya pembejeo.
Kwa upande wake, Afisa kilimo kituo cha Rasilimali cha kilimo Mwendakulima kinachofadhiliwa na Kampuni ya Barrick, Yusuf Sifaeli, alisema baada ya Mgodi wa Buzwagi kumaliza Shughuli zake za uzalishaji dhahabu ulifanya utafiti kwa wananchi wa maeneo yanayozunguka mgodi huo na kubaini shughuli kuu za kiuchumi zinazotegemewa na wananchi ni kilimo ndipo mgodi ukaamua kuanzisha kituo hicho
“Mpaka sasa tumeweza kufundisha wakulima wapatao 4,200 tangu mwaka 2019 juu ya kilimo bora cha mazao ya Mahindi, Mpunga na alizeti, mkulima aliyekuwa anazalisha gunia tatu hadi tano za mahindi kwa ekari moja sasa anapata gunia 25”, alisema Sifaeli.
Mmoja wa wakulima aliyenufaika kupitia kituo ,Bertha Yohana, kutoka kata ya Mwendakulima, akiongea kwa niaba ya wenzake ameipongeza Serikali kupitia Halmashauri ya Manispaa ya Kahama pamoja na Kampuni Barrick kupitia kituo hicho kwa kubuni na kuleta utaratibu wa ukopeshwaji wa pembejeo ambao umbao unaendelea kuwanufaisha.
Diwani wa kata ya Mwendakulima Adulrahman Hassan, ameishuruku Manispaa ya Kahama na kampuni ya Barrick kwa kuanzisha mradi huo na kuahidi kuwahamasiaha wakulima pindi watakapovuna mazao yao kuhakikisha wanarejesha mikopo yao.
No comments: