LIVE STREAM ADS

Header Ads

Nchimbi ateuliwa Katibu Mkuu CCM

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu, Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Katibu Mkuu mpya wa Chama cha Mapinduzi CCM, Ndugu Emmanuel John Nchimbi baada ya kuteuliwa kushika wadhifa huo kwenye Kikao Maalum cha Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kilichokutana tarehe 15 Januari, 2024 Mjini Unguja Zanzibar.

Dkt. Emmanuel Nchimbi ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) akichukua nafasi ya Daniel Chongolo aliyejiuzulu.

Uteuzi wa aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Misri, Dk Emmanuel Nchimbi kuwa Katibu Mkuu wake mpya umefanyika leo Jumatatu Januari 15, 2024 wakati wa kikao cha Kamati Kuu ya CCM kisha kuthibitishwa na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC) iliyofanyika mjini Unguja, Zanzibar.

No comments:

Powered by Blogger.