LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wafanyabishara wadogo Mwanza waomba vyoo minadani

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Wafanyabiashara wadogo maarufu mkoani Mwanza wameiomba Serikali kuboresha miundombinu katika minada kwa kuwajengea vyoo ili waweze kufanya biashara katika mazingira salama.

Ombi hilo limetolewa Alhamisi Januari 25, 2024 na Mwenyekiti wa wafanyabiashara katika masoko na minada mkoaniMwanza, Jastine Sagara wakati akizungumza kwenye kikao cha utoaji wa elimu ya usafi wa mazingira kilichofanyika kwenye mnada wa Kitangiri wilayani Ilemela.

Sagara ameeleza kuwa mnada wa Kitangiri ni miongoni mwa mnada kongwe lakini tangu wameanza kufanya biashara hakuna huduma ya choo hivyo wafanyabiashara kulazimika kwenda kujisaidia kwenye nyumba ya mtu binafsi.

"Siku akisafiri au wafanyabiashara wakimuudhi na akaamua kufunga choo chake tutakosa sehemu ya kujistri hivyo mazingira yetu yatachafuka kutokana nawatu kujisaidia hovyo tunaiomba Serikali itujengee choo ili tuwe na huduma hiyo ya kudumu" amesema Sagara.

Amesema katika kipindi hiki cha mlipuko wa kipindupindu Serikali inahimiza suala la usafi kwenye masoko, minada na utoaji elimu hivyo wanapaswa kuwawekea miundo mbinu rafiki ili waweze kuepukana na magonjwa hayo ikiwemo kipindupindu.

Baadhi ya wafanyabiashara wameeleza kuwa licha ya wao kuwa sehemu ya wachangiaji katika pato la Taifa bado miundombinu katika maeneo yao ya kazi hususani choo imekuwa changamoto hali inayopelekea kushindwa kufanya shughuli zao kwa amani.

"Tunawaomba viongozi wa Serikali waliopata dhamana kuweka utaratibu wa kutembelea katika maeneo ya minada ili kuweza kuona na kutatua changamoto mbalimbali zinazotukabili" wamesema.

Akijibu suala la ukosefu wa miundombinu ya choo katika mnada huo, Afisa Mtendaji wa Mtaa wa Kitangiri, Stella Kilawe amesema kero ya ukosefu wa choo imefikishwa katika vikao vya Kamati ya Maendeleo ya Kata (WDC) kwa ajili ya kuweka msisitizo wa kuboreshewa mnada huo ili uwe katika hali ya usafi.

"Nimuombe mweshimiwa Diwani aende akaongee na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela kwa ajili ya utekelezaji wa ujenzi wa miundombinu ya choo, hivyo tunaomba muendelee kuwa wavumilivu wakati suala hili linatafutiwa ufumbuzi" amesema Kilawe.
Na Hellen Mtereko, Mwanza
Mwenyekiti wa wafanyabiashara wadogo katika masoko na minada mkoani Mwanza, Jastine Sagara akizungumza katika mnada wa Kitangiri wilayani Ilemela kwenye kikao kilicholenga kutoa elimu kuhusu usafi wa mazingira katika mnada huo.
Afisa Mtendaji Kata ya Kitangiri wilayani Ilemela, Stella Kilawe akizungumza na wafanyabishara wadogo katika mnada wa Kitangiri kuhusu umuhumu wa kuzingatia usafi ili kuondokana na magonjwa ya milipuko.

No comments:

Powered by Blogger.