LIVE STREAM ADS

Header Ads

Waziri Mavunde aridhishwa na uendeshaji wa kiwanda cha dhahabu Mwanza

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Waziri wa Madini, Antony Mavunde amefanya ziara ya kukagua kiwanda cha kusafisha dhahabu cha Mwanza Precious Metal Refinery kilichopo eneo la Sabasaba Manispaa ya Ilemela na kuridhishwa na uendeshaji wa kiwanda hicho.

Mavunde amefanya ziara hiyo Alhamisi Januari 04, 2024 ambapo amelipongeza Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kwa kushirikiana na mwekezaji kampuni ya Rozella kutoka nchini Dubai kwa usimamizi na uendeshaji mzuri wa kiwanda hicho.

Amesema lengo la Serikali inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kuhakikisha madini yanawanufaisha watanzania hivyo kabla ya kusarishishwa nje ya nchi sharti yaongezewe thamani hapa hapa nchini.

Awali akitoa taarifa ya usimamizi na uendeshaji wa kiwanda hicho, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu STAMICO, Deusdedith Magala ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya uendeshaji wa kiwanda hicho amesema mradi huo unatarajiwa kuleta mapinduzi makubwa katika sekta ya madini hapa nchini ikiwemo kutoa fursa kwa benki kuu BOT kununua dhahabu iliyosafishwa.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.