LIVE STREAM ADS

Header Ads

Alamba mchongo akisherehekea siku yake ya kuzaliwa

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Kwa mara nyingine tena mkoa wa Ruvuma umejipatia mshindi wa Mchongo Jackpot ya Shillingi 250,000,000.00 baada ya Bernard M. aliyejinyakulia ushindi huu Disemba 2023 na wakati huu ni Peter L. kutoka Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma kupitia kampuni ya michezo ya kubashiri ya (BetwayTanzania).

Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhiwa hundi yenye kiasi hicho cha fedha katika hafla iliyofanyika katika Ofisi za Betway Tanzania jijini Dar es Salaam, Ndugu, Peter L. Milionea huyo mpya amesema “Imekuwa kama ndoto kupata kiasi hicho cha fedha kwenye siku yangu yakuzaliwa”, ambacho anadai hakutegemea hata siku moja kama angeweza kuja kuwa mshindi na kuingia katika kundi la matajiri nchini huku akiwasisitiza wananchi wengine kushiriki katika kubashiri na michezo mingine inayoendeshwa kupitia kampuni hiyo ya Betway Tanzania.

Ameushukuru uongozi mzima wa kampuni ya (Betway Tanzania) kwa ushirikiano waliuonyesha tangu alipotangazwa kuwa mshindi hadi hatua ya kukabidhiwa fedha zake huku akisisitiza kuwa ataendelea kubashiri zaidi na zaidi kupitia kampuni hiyo kwa kuwa inaaminika.

Kwa upande wake Meneja Masoko Betway Tanzania, Calvin Mhina mbali na kumpongeza mshindi huyo amesema kampuni hiyo imekuwa karibu na wateja wake wakati wote huku akisisitiza kuwa ushindi na malipo kwa mshindi huyo ni kielelezo cha uaminifu wa kampuni hiyo.

Amesema wao kama kampuni bora ya michezo ya kubashiri Tanzania na Duniani kote ushindi huo unawafanya kuendelea kujiweka mbele zaidi hasa kwa kuwa na promosheni nyingi nzuri zinazomuwezesha mtu kushinda kwa urahisi.

No comments:

Powered by Blogger.