LIVE STREAM ADS

Header Ads

Naibu Waziri Kapinga aipongeza ORYX Gas kwa kuhamasisha matumizi ya gesi

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Kampuni ya Oryx Gas kwa kushirikiana na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kilimanjaro Shally Raymond wamekabidhi mitungi ya gesi ya kupikia 1000 pamoja na majiko yake bure kwa viongozi wa madhehebu ya dini mbalimbali pamoja na wajasiriamali mkoani Kilimanjaro ,lengo likiwa kulihusisha kundi kulinda na kutunza mazingira kwa kutotumia kuni na mkaa.

Akizungumza katika hafla ya ugawaji wa mitungi hiyo ya gesi iliyofanyika katika Chuo cha Polisi(CCP) mkoani Kilimanjaro, Naibu Waziri wa Nishati Judith Kapinga ambaye alikuwa mgeni rasmi ameeleza kwa kina kuhusu umuhimu wa viongozi wa dini kushiriki katika kuihamasisha jamii kutumia nishati safi ya kupikia.

Amefafanua viongozi wa dini ni watu wa thamani sana na watu wanawathamini na kuwasikiliza, hivyo viongozi wetu wa dini wanayo nafasi kubwa ya kushiriki katika kampeni ya kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupika sambamba na kuendelea kuiambia jamii isiendelee kutumia kuni na mkaa ili kuepuka kuharibu mazingira kwa kukata miti.

“Tunamatumaini matumaini makubwa na viongozi wa dini na ndio ambao wanaweza kutusaidia kuwaelimisha na kuwaambia wananchi kuhusu kutunza mazingira” amesema Naibu Waziri Kapinga na kusisitiza watu wengine ambao hawana sura ya kimungu ni ngumu kuaminika kwa jamii.

Amesisitiza kiongozi wa dini akisema msikate miti watu wanaamini huyo ametumwa na Mungu hivyo hawataka miti huku akifafanua uharibifu wa mazingira unatokana na ukataji miti imessababisha hata mikoa iliyokuwa na mvua nyingi kama mikoa ya nyanda za juu kusini ambazo zilitakiwa mvua kuanza Novemba zinaanza mwishoni mwa Desemba.

“Kwa nini, kwa sababu ya matendo yetu wenyewe ya kuharibu mazingira, hivyo tunaamini viongozi wa dini mpo katika nafasi ya kutusaidia kuendelea kukumbusha jamii kwamba dunia hii ambayo tumepewa zawadi na Mwenyezi Mungu ni haki ya kila mmoja kuilinda leo, tunawatoto na wajukuu na tutakuwa na vitukuu pia, sasa kama rasilimali zote tulizonazo tutazichezea leo hawa wajuu na vitukuu vitaishi katika mazingira gani”

Pia amesema kuwa katika kampeni hiyo ya kuhamasisha matumizi ya nishati ya kupikia wamekuwa wakihusisha zaidi wanwake kwasababu wanawake ndio wanaokaa jikoni kupika kuandaa chakula. “Mwaka 2024 tusikubali kupika kwa kuni wala mkaa, tunashukuru sana oryx kwa kutupatia majiko ya gesi”.

Kuhusu kampeni ya nishati safi ya kupikia, amesema mwishoni mwa mwaka jana kulikuwa na mkutano wa dunia wa mazingira ambapo Rais Dk.Samia Suluhu Hassan alienda na ajenda mahususi ya kumkomboa mwanamke wa Afrika sio mwanamke wa Tanzania peke yake.

“Kwa hiyo ndgu zangu tunapozungumzia nishati safi ya kupikia tunazungumzia mambo ambayo yamebebwa ndani ya moyo wa Rais Dk.Samia Suluhu Hassan, ni ajenda yake ambayo yeye mwenyewe ameibeba. Tunapozungumzia wanawake wa Afrika tunazungumzia na wanawake wa Tanzania ,kwa hiyo kwa lugha nyepesi wanawake wa Tanzania ndio wabeba bendera wa kumsaidia Rais kwenye ajenda hii ya nishati safi ya kupikia ili tuwe mfano kwa mataifa mengine” amesema.

Kwa upande wake Meneja Mauzo wa Kampuni ya Oryx Gas Tanzania Shaban Fundi aliyemwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo Benoite Araman ametumia nafasi hiyo kueleza kuwa kwa muda mrefu sasa wamekuwa wanajivunia kuwezesha makundi mbalimbali yakiwemo wanawake, watoto na wajasiriamali kupata nishati safi ya kupikia.

“Kufanya hivyo tunaamini tunaikomboa jamiina taifa kwa ujumla wake kwani kupika kwa gesi ya Oryx kuna maanisha kuboresha afya za kinamama kwa kueuka kuvuta moshi mbaya wa kuni na mkaa.Pia tunaweza watoto kupata muda wa kwenda shule badala ya kutumwa kutafuta kuni” amesema Fundi.

Amesisiza kampuni hiyo kwa kutambua nafasi ya viongozi wa dini imeona ni vema sasa ikatoa mitungi ya gesi ya Oryx na majiko yake kwa kundi hilo sambamba na kuelezea kwa kina umuhimu wa kutunza mazingira na wanaamini kuwa viongozi wa dini wana nafasi kubwa ya kusema na kusikilizwa, hivyo watakapokuwa mabalozi wa kuzungumzia nishati safi ya kupikia jamii itabadilika na hivyo kuokoa mazingira.

Aidha amekumbusha kuwa mwaka 2021 Rais Dk.Samia Suluhu Hassan alianzisha kampeni ya nishati safi ya kupikia na alitoa maono yake ya kwamba ifikapo mwaka 2032 asilimia 80 ya wananchi itumie nishati safi, hivyo kuanzia hapo Oryx iliongeza nguvu na hadi sasa ya mitungi 19000 bure yenye thamani isiyopungua Shilingi bilioni 1.5.
Naibu Waziri wa Nishati Judith Kapinga akizungumza katika hafla ya kukabidhi mitungi ya kupikia ya Oryx 1000 kwa viongozi wa dini mbalimbali pamoja na wajasiriamali Mkoa wa Kilimanjaro.
Meneja Masoko wa Kampuni ya Oryx Gas Peter Ndomba akitoa elimu ya kutambua mtungi wa gesi ambao umepata hitilifu na hatua zinazoweza kuchukuliwa ili usilete madhara kwa mtumiaji huku akieleza kuwa kampuni hiyo imekuwa ikihimiza matumizi salama ya majiko ya gesi.
Naibu Waziri wa Nishati Judith Kapinga (wa tatu kushoto) akiwa na Mbunge wa Jimbo la Moshi Mjini Priscus Tarimo (wa kwanza kushoto), Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM)Mkoa wa Kilimanjaro (wa pili kulia) na Meneja Masoko wa Oryx Shaban Fundi (wa kwanza kulia) wakimkabidhi mtungi wa gesi ya kupikia ya Oryx Ofisa Daawa Manispaa ya Moshi Shekhe Hashim Mmbaga wakati wa hafla ya kukabidhi mitungi ya kupikia ya Oryx 1000 kwa viongozi wa dini mbalimbali pamoja na wajasiriamali Mkoa wa Kilimanjaro.
Naibu Waziri wa Nishati Judith Kapinga( mwenye nguo nyeupe) akiwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Kilimanjaro (wa pili kulia) na Meneja Masoko wa Oryx Shaban Fundi( wa kwanza kulia) wakimkabidhi mtungi wa gesi ya kupikia ya Oryx Mwenyekiti wa Kanda ya Sita KKKT Dayosisi ya Kaskazini, Usharika wa Kyomu mkoani Kilimanjaro Mchungaji Fredrick Minja.
Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga (wa tatu kushoto) akimkabidhi mtungi wa gesi ya kupikia ya Oryx Ofisa Daawa wa Kata ya Msaranga iliyopo Moshi Mjini Shekhe Twahir Hussein.
Naibu Waziri wa Nishati Judith Kapinga akiwasha moto katika jiko la gesi la Oryx wakati wa hafla ya kukabidhi mitungi ya gesi na majiko yake kwa viongozi wa dini pamoja na wajasiriamali wa Mkoa Kilimanjaro.
Naibu Waziri wa Nishati Judith Kapinga akizungumza katika hafla ya kukabidhi mitungi ya kupikia ya Oryx 1000 kwa viongozi wa dini mbalimbali pamoja na wajasiriamali mkoani Kilimanjaro.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Kilimanjaro, Patrick Boisafi akizungumza katika hafla hito.
Mbunge wa Jimbo la Moshi Mjini Priscus Tarimo akizungumza katika hafla ya kukabidhi mitungi ya kupikia ya Oryx 1000 kwa viongozi wa dini mbalimbali pamoja na wajasiriamali Mkoa wa Kilimanjaro.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kilimanjaro Shally Raymond akizungumza katika hafla ya kukabidhi mitungi ya kupikia ya Oryx 1000 kwa viongozi wa dini mbalimbali pamoja na wajasiriamali Mkoa wa Kilimanjaro.
Meneja Mauzo wa Kampuni ya Oryx Gas Shaban Fundi akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo Benoite Araman katika hafla ya kukabidhi mitungi ya kupikia ya Oryx 1000 kwa viongozi wa dini mbalimbali pamoja na wajasiriamali Mkoa wa Kilimanjaro.
Viongozi wa dini kutoka madhehebu mbalimbali mkoani Kilimanjaro wakiwa makini kupata maelezo ya umuhimu wa kutumia nishati safi ya kupikia katika hafla ya kukabidhi mitungi ya kupikia ya Oryx 1000 kwa viongozi wa dini mbalimbali pamoja na wajasiriamali Mkoa wa Kilimanjaro.
Meneja Masoko wa Kampuni ya Oryx Gas Peter Ndomba akitoa elimu ya kutambua mtungi wa gesi ambao umepata hitilifu na hatua zinazoweza kuchukuliwa ili usilete madhara kwa mtumiaji huku akieleza kuwa kampuni hiyo imekuwa ikihimiza matumizi salama ya majiko ya gesi.
Naibu Waziri wa Nishati Judith Kapinga akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa dini wakati wa hafla ya kukabidhi mitungi ya kupikia ya Oryx 1000 kwa viongozi wa dini mbalimbali pamoja na wajasiriamali Mkoa wa Kilimanjaro.
Na Emmanuel Mbatilo

No comments:

Powered by Blogger.