LIVE STREAM ADS

Header Ads

Michezo ya kubahatisha sio ajira- Mkurugenzi Mkuu GBT

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT), James Mbalwe Akizungumza katika kikao kazi kilichowakutanisha maofisa wa Bodi hiyo, waandishi na wahariri wa vyombo vya habari Jijini Dar es Salaam.

Na Chalila Kibuda, Michuzi Blog
Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha (GBT), James Mbalwe sekta ya michezo inakua na kuchangia maendeleo ya kiuchumi.

Mbalwe ameyasema hayo wakati wa kikao cha Wahariri na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam.

Amesema michezo ya kubahatisha ni michezo kama mingine na hakuna nia kutaka vijana waharibiwe.

Mbalwe amesema kuwa mchezo wa kubahatisha baadhi wamekuwa wakinyanyapaa na kutaka kuwa GBT ipo kisheria na inadhibitiwa.

Amesema kuwa katika kodi yamepanda kutoka kodi Bilioni 33.3 hadi kufikia kodi bilioni ya 170.4 na wanatarajia kukusanya kodi ya bilioni 200 kwa mwaka wa fedha unaoishia 2023/2024.

Amesema katika ushirikiano usimamizi na udhibiti wa sekta na vyombo Ulinzi na Usalama y ili kudhibiti wavunjaji wa sheria ya michezo ya kubahatisha nchini.

Amesema wanaona umuhimu wa kutoa elimu mara kwa mara kwa vile GBT ni taasisi kwa miaka 20 hivyo wajibu.

Alisema semina hizi na watu muhimu wa vyombo vya habari kama hizo zimekuwa na manufaa makubwa katika kurahisisha utendaji wa GBT.

“Kazi yetu ni udhibiti, kusimamia na kuratibu uendeshaji wa michezo ya kubahatisha nchini na haifanyi biashara na iko chini ya Wizara ya Fedha chini ya Msajili wa Hazina” alifafanua.

Bw. Mbalwe alimeelezakuimarisha ushirikiano katika usimamizi wa sekta na hivyo tunaomba kamati ya usalama ya mkoa kuongeza ushirikianoz aidi katika kudhibiti wavunja sharia ya Michezo ya Kubahatisha.

“Nina sisitiza Michezo ya Kubahatisha ni Burudani na sio Ajira au njia ya kujitafutia kipato” alifafanua Mbalwe.

Kuanzishwa kwa GBT kumewezesha sekta ya michezo ya kubahatisha kuratinbiwa vizuri zaidi na iweze kuchangia ipasavyo katika pato la taifa na wananchi wanaojishughulisha kwenye michezo hiyo wanalindwa ipasavyo.

“Sekta inakuwa kwa kasi na kwa sababu hiyo kunahitaji uratibu makini ili iendelee kukua katika namna ambayo utaratibu unaopasa bila kupoteza malengo ya msingi ya kuanzishwa kwake” alifafanua Mbalwe.

Amesema kuwa mwaka wa fedha unaoishia Jalai watafika bilioni 200 kutokana kwa miazi mitatu kuanzia Agasti hadi Desemba zaidi ya bilioni 100 zimepatikana.

Amesema ajira zilizozaliswa Sekta ya michezo yakubahatisha Tanzania
imefanikiwa kuzalisha ajira zilizo rasmi na zisizo rasmi zaidi ya 25,000.

Mbalwe amesema kuwa GBT hadi sasa imesajili kampuni 91 za michezo ya kubahatisha.

Amesema ongezeko la Mapato ya Serikali yatokanayo na Kodi ya
biashara ya michezo ya kubahatisha yamekuwa yakiongezeka mwaka hadi mwaka na hiyo kutokana udhibiti wa michezo.

Amesema ajira zilizozaliswa Sekta ya michezo yakubahatisha Tanzania
imefanikiwa kuzalisha ajira zilizo rasmi na zisizo rasmi zaidi ya 25,000.
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodaus Balile, akizungumza katika kikao cha wahariri na Bodi ya Michezo ya kubahatisha (GBT) Jijini Dar es Salaam.
Afisa Habari Mwandamizi wa Ofisi ya Msajili wa Hazina Sabatho Kosuri, akizungumza kuhusiana na vikao kazi kati ya Taasisi zilizochini ya Msajili wa Hazina ,jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wahariri na waandishi wa habari katika mkutano wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha (GBT).

No comments:

Powered by Blogger.