Dkt. Biteko aweka jiwe la msingi ujenzi wa makao makuu ya kanisa la AICT
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la Makao makuu ya kananisa la AICT lililopo eneo la Makongoro jijini Mwanza.
Biteko ameweka jiwe hilo Jumamosi Machi 16, 2024 kwa niaba ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko akizungumza kwa niaba ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan (hayuko pichani) wenye ibada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la Makao Makuu ya Kanisa la AICT eneo la Makongoro jijini Mwanza.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko akizungumza kwa niaba ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan (hayuko pichani) wenye ibada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la Makao Makuu ya Kanisa la AICT eneo la Makongoro jijini Mwanza.
Viongozi mbalimbali meza Kuu wakifuatilia hotuba ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko.
Askofu Mkuu Kanisa la AICT, Mussa Magwesela akiongoza maombi wakati wa ibada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la Makao Makuu ya Kanisa hilo eneo la Makongoro jijini Mwanza.
Askofu Mkuu Kanisa la AICT, Mussa Magwesela akiongoza maombi wakati wa ibada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la Makao Makuu ya Kanisa hilo eneo la Makongoro jijini Mwanza.
Viongozi mbalimbali wa kanisa la AICT akiwemo Askofu Mkuu wa pili wa kanisa hilo, Methuselah Nyagwasa (wa kwanza kushoto).
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko (kulia) akiwa na Askofu Mkuu Kanisa la AICT, Mussa Magwesela (mwenye fimbo) pamoja na viongozi mbalimbali waliohudhuria ibada hiyo.
Mkuu wa Wilaya Nyamagana, Amina Makilagi akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Mwanza, Amos Makalla (hayuko pichani).
Mkuu wa Wilaya Nyamagana, Amina Makilagi akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Mwanza, Amos Makalla (hayuko pichani).
Mwonekano (kulia) baada ya ujenzi kukamilika.
***
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko amewataka viongozi wa Serikali katika maeneo mbalimbali nchini kuhakikisha wanatatua kero za wananchi kwa wakati badala ya kuzichukua bila ya kuzifanyia kazi.
Dkt. Biteko ametoa agizo hilo wakati akimwakilisha Rais Dkt. Samia
Suluhu Hassan katika Hafla ya kuweka jiwe la msingi jengo la ofisi za makao Makuu ya Africa Inland Church Tanzania (AICT) jijini Mwanza.
Dkt. Biteko ametoa agizo hilo kufuatia risala ya Askofu Mkuu AICT, Mussa Magwesela liyoweka wazi kasi nsogo ya utatuzi wa changamoto zinazolitatiza Kanisa hilo kwa muda mrefu bila kupatiwa majibu wala utatuzi.
Dkt. Biteko amesema mbali na agizo la Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango la kushughulikia hoja ya AICT kuhusu umiliki wa Shule za Sekondari za Bulima na Kahunda pamoja kiwanja kilichopo jijini Mwanza katika eneo la Makongoro lakini agizo hilo bado halijashughulikiwa.
"Hili suala la Kahunda na Bulima nataka niwahakikishie kwamba
tunalitambua na tunalifanyia kazi, lakini hili la umiliki wa kiwanja
sifurahishwi na kasi ya ndogo ya ushughulikiaji, haiwezekani jambo
hili kutoka Makamu wa Rais alitolee maelekezo mwezi Januari mwaka 2023
hakuna majibu hadi leo, kama ombi la Kanisa haliwezekani au linawezekana wapeni majibu wahusika" amesema Dkt. Biteko
Dkt. Biteko amemwagiza Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi pamoja na Halmashauri ya Jiji la Mwanza kukutana chini usimamizi wa Mkuu wa Mkoa siku ya Ijumaa (tarehe 22 Machi 2024) washughulikie
suala hilo na wahusika wapewe majibu ya changamoto husika.
Kuhusu ombi la AICT la kulipwa fedha wanazodai Mfuko wa Bima ya Afya
(NHIF) takribani shilingi milioni 181, Dkt. Biteko amesema kuwa kabla
ya mwisho wa mwezi huu fedha zote zitakuwa zimelipwa na hii ni baada
ya kufanya mazungumzo na Wizara ya Afya.
Aidha kuhusu ombi la kanisa hilo la kuwekewa mfumo wa majitaka amesema litafanyiwa kazi kupitia Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa
Mazingira Mwanza (MWAUWASA).
Dkt. Biteko amesema kuwa, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anatambua
kuwa Serikali peke yake haiwezi kupeleka maendeleo kwa wananchi wote kwa wakati hivyo madhehebu ya dini yana mchango wake katika
maendeleo.
Amesema Rais anatambua kuwa ili kuwa na jamii ya watu waliostaarabika
na kuheshimika elimu ni jambo la msingi lakini pia nyumba za ibada
zina umuhimu mkubwa katika kukuza watu kimaadili.
Ameongeza Rais Dkt. Samia yupo tayari muda wowote kuwasilikiza viongozi wa dini na kuchukua ushauri wao na kwamba anaamini katika maridhiano na kujenga Taifa lenye umoja.
Awali, Baba Askofu Mkuu wa AICT, Mussa Magwesela alisema kuwa, Kanisa linatambua juhudi za Serikali katika kuwaletea maendeleo wananchi
pamoja na ustawi wa kijamii na hivyo AICT itaendelea kuunga mkono juhudi hizo za Serikali kwa kutoa huduma mbalimbali kwa jamii ikiwemo
kwenye Elimu na Afya pamoja na kuendelea kuhubiri amani, mshikamano na umoja.
Amesema kanisa hilo pia linaendelea kutoa elimu ya ujasiriamali katika maeneo mbalimbali nchini ili kuwakwamua wananchi kiuchumi,
kwani AICT inatambua kuwa mwanadamu si roho pekeyake bali ana mwili wenye mahitaji mbalimbali.
Ameongeza kuwa AICT pia itaendelea kushikamana na Serikali katika kupinga vitendo vyote ambavyo ni kinyume na maadili ya kitanzania.
Vilevile Askofu Magwesela amesisitiza kuhusu umoja, uwazi,
uwajibikaji, uadilifu na uaminifu katika utendaji kazi wa kila siku ili kutekeleza kwa ufanisi mipango inayowekwa ndani na nje ya Serikali.
Kanisa la AICT lilianzishwa miaka 115 iliyopita makao makuu
yakiwa jijini Mwanza.
PIA SOMA>>> Dkt. Biteko amwakilisha Rais Samia Mwanza
No comments: