LIVE STREAM ADS

Header Ads

MisaTan, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora wasaini mkataba wa ushirikiano

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Patience Ntwina (kushoto) akibadilishana nyaraka na Mkurugenzi Mtendaji wa MISA TAN, Elizabeth Riziki baada ya kutia saini mkataba wa ushirikiano baina ya taasisi hizo mbili.
Mwenyekiti wa bodi na Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Amina Talib Ali akipongezana na Mkurugenzi Mtendaji wa MISA TAN Bi. Elizabeth Riziki (kushoto) baada ya kutia saini mkataba wa ushirikiano baina ya taasisi hizo mbili.
****


Taasisi ya vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika Tawi la Tanzania (MISA-TAN) na Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora wamesaini mkataba wa miaka mitatu (2024- 2027) wa ushirikiano makubaliano ya kufanya kazi kwenye maeneo mbalimbali ya haki za binadamu na hasa haki za waandishi wa habari na wananchi kwa ujumla.

Hafla ya utiaji saini Mkataba huo imefanyika jijini Dodoma
na kuhudhuriwa na Mwenyekiti wa bodi na Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Amina Talib Ali, Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Mhe. Mohamed Khamis Hamad, Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Patience Ntwina, Makamishina, wakurugenzi wa tume na kwa Upande wa MISA TAN, Makamu Mwenyekiti wa MISA TAN, James Marenga na Mkurugenzi Mtendaji wa MISA TAN, Elizabeth Riziki.

No comments:

Powered by Blogger.