LIVE STREAM ADS

Header Ads

TGNP waguswa na tukio la baba kuwabaka watoto wake

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Wadau wa maendeleo kwa kushirikiana na Serikali wameitaka jamii kuendelea kukemea vikali vitendo vya ukatili vinavyofanywa na baadhi ya watu wasiokuwa waadilifu jambo ambalo linapelekea kuongezeka kwa mmong'onyoko wa maadili na kuacha baadhi ya familia kukosa malezi na kuwa na hali ya tegemezi Nchini.

Akizungumza Machi 13, 2024 Jijini Dar es Salaam wakati wadau wa kupinga ukatili wa kijinsia kutoka Ethiopia walipotembelea Kituo cha Taarifa na Maarifa Kata ya Majohe kwa lengo la kujifunza na kubadilishana changamoto za ukatili,wanachama wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Rehema Mwateba amesema wakati umefika wa kuzungumza ukweli kuhusu ukatili unaofanyika.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kituo Cha Taarifa na Maarifa Kata ya Majohe, Tabu Ally amesisitiza umuhimu wa kuwachukulia hatua za kisheria wahusika wa matukio hayo na akienda mbali zaidi kuiomba serikali kuweka sheria kali juu ya watu ambao wameendelea kufanya vitendo visivyo rafiki katika jamii husika.

Aidha aliongeza kuwa kuna hitajika jitihada za wadau mbalimbali wa maendeleo na serikali kutoa elimu kwa baadhi ya watu ambao bado wanauelewa mdogo kwenye masuala ya haki ya binadamu ili kupunguza vitendo vya ukatili, pia amewataka watumishi wa umma wakiwemo mawaziri, wabunge na viongozi wengine wa ngazi za juu kutembea kwenye majimbo hasa ya ngazi za nchini ili kujionea vitendo vya kikatili vinavyozidi kushamiri hasa kwa watoto wa kike wenye umri mdogo.

Naye Mkazi wa Mtaa wa Kivule Majohe, Wivina Alkadi ambaye alifanyiwa ukatili na mume wake kwa kuwabaka wanaye wawili na mmoja kumpa ujauzito jambo ambalo lilipelekea mtuhumiwa huyo kufungwa kifungo cha miaka 60 jela, ameiomba jamii kumsaidia baadhi ya mahitaji ya familia kwani anaishi katika mazingira magumu.

Pia ametumia fursa hiyo kuomba Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na watanzania kiujumla kumsaidia ili watoto wake waweze kuendelea na masomo kwani wananishindwa kusoma kutokana na hali ya maisha ambayo amekuwa akiyapitia mama huyo mara baada tu ya mume wake kuhukumiwa kifungo cha miaka 60 jela.

Huku wadau wa kupinga ukatili wa kijinsia kutoka Ethiopia akiwemo Rediet Asfew wamesema kuwa wataendelea kutoa ushirikiano kwa TNGP katika kufanya uwezeshaji wa kiuchumi kwa Wanawake ili kuunga mkono jitihada mbalimbali zinazofanywa na wadau na serikali katika kuhakikisha masuala ya ukatili yanadhibitiwa ili kumkwamua mwanamke kiuchumi .

No comments:

Powered by Blogger.