LIVE STREAM ADS

Header Ads

Viongozi, wajumbe CHADEMA wamchukulia Wenje fomu kutetea nafasi yake

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Viongozi wa Majimbo, Wilaya na Mikoa ambao ni wajumbe wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Victoria wamemchukulia fomu ya Mwenyekiti wa Kanda hiyo, Ezekiel Wenje ili kutetea nafasi hiyo kwa awamu ya pili.

Viongozi na wajumbe hao ambao ni 54 kati ya 79 kutoka majimbo 25 ya uchaguzi wamefika katika ofisi za Kanda hiyo zilizoko Kata ya Nyegezi jijini Mwanza kwa ajili ya kutekeleza zoezi la kumchukulia fomu hiyo, Jumanne Aprili 16, 2024.

Khalid Hussein ambaye ni Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Muleba mkoani Kagera na pia mgombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Kanda ya Victoria katika uchaguzi wa kuchagua viongozi mbalimbali wa Kanda hiyo utakaofanyika hivi karibuni amesema, ndugu Ezekiel Wenje amekuwa akifanya kazi kwa ufanisi na weledi ndiyo maana bado wanamuhitaji ili azidi kuwaongoza.

"Pamoja na kumchukulia fomu ndugu Ezekiel Wenje, mimi pia nimechukua fomu ya kuwania nafasi ya Makamu Mwenyekiti Kanda ya Victoria ili niendelee kuipeperusha bendera ya CHADEMA" amesema Hussein.

Awali Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Geita, Deogratius Shinyanga amesema Ezekiel Wenje amekuwa mwaminifu kwenye chama hajawahi kurudi nyuma katika kutekeleza majukumu ya chama.

"Kuna watu tuliwaamini kwa kiwango kikubwa lakini mwisho wa siku walitufedhehesha kwa kuwa na tamaa mbalimbali ikiwemo fedha lakini Ezekiel Wenje amekuwa ni mwaminifu na msikivu na ameamua kusimamia na chama hata kwenye nyakati ngumu ambazo tumekuwa tukizipitia" amesema Shinyanga.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa CHADEMA (BAZECHA) Mkoa Mwanza, Japheth Nungwana amewaasa wagombea kuwa watulivu kuelekea kwenye uchaguzi huo hatua itakayosaidia kuepusha makundi yatakayoweza kuwagawanya.
Na Hellen Mtereko, Mwanza 
Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Muleba mkoani Kagera, Khalid Hussein (kushoto) akimchukulia fomu ya Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Victoria, Ezekiel Wenje (hayuko pichani) ili kuwania tena nafasi hiyo ambayo baada ya muda wake wa uongozi wa sasa kukoma hivi karibuni. Kulia ni Afisa wa chama hicho, Hemed Sombi.
Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA (BAZECHA) Mkoa Mwanza, Japheth Nungwana akizungumza kwenye zoezi la kumchukulia fomu Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Victoria, Ezekiel Wenje (hayuko pichani) ambaye uongozi wake unakaribia kuisha.
Baadhi ya wanachama wa CHADEMA Kanda ya Victoria waliojitokea jijini Mwanza kumchukulia fomu Mwenyekiti wa Kanda hiyo, Ezekiel Wenje (hayuko pichani) ili kuwania tena nafasi yake baada ya muda kufikia uko hivi karibuni.

No comments:

Powered by Blogger.