LIVE STREAM ADS

Header Ads

CHADEMA Kanda ya Victoria wamtaka tena Wenje

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Viongozi na wajumbe wa CHADEMA kutoka majimbo 25 ya Kanda ya Victoria wamejitokeza kumchukulia fomu Mwenyekiti anayemaliza muda wake, Ezekia Wenje ili kugombea tena nafasi hiyo baada ya kumaliza muda wake.

Viongozi na wajumbe hao wapatao 54 kati ya 79 wamefika katika ofisi za Kanda ya Ziwa Victoria zilizopo Nyegezi jijini Mwanza huku wakielezea kuwa na imani na Wenje.

"Wenje amekuwa mwaminifu sana kwenye chama chetu, hata katika nyakati ngumu hakuonesha usaliti, aliendelea kulinda heshima ya CHADEMA hivyo tunamtaka agombee tena ndiyo maana tumeamua kumchangia na kumchukulia fomu" amesema Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa CHADEMA Mkoa Mwanza, Japheth Nungwana.

No comments:

Powered by Blogger.