LIVE STREAM ADS

Header Ads

Chama apewa zawadi ya nguruwe

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Mkurugenzi wa kampuni ya Kijiji cha Nguruwe kilichopo Zamahero wilaya ya Bahi mkoani Dodoma ambaye ni shabiki kindakindaki wa timu ya Simba SC Simon Mnkondya ametekeleza ahadi yake aliyoahidi endapo Simba ingepata magoli katika mechi yake dhidi ya timu ya Ihefu SC yenye maskani yake mkoani Singida.

Mkondya ambaye ni Mkurugenzi wa .akampuni ya kimataifa ya kilimo cha Vanilla duniani alitoa ahadi zawadi ya nguruwe mmoja mkubwa aina ya Large White mwenye kilo 500 sawa na shilingi Milioni tatu kwa kila goli ambalo lingefungwa na Simba SC katika mchezo wake na Ihefu SC wa Jumamosi Aprili 13, 2024 katika uwanja wa Iliti Singida.
Akizungumza na vyombo vya habari jijini Arusha, Jumapili Aprili 14,204 Mkondya amesema atatoa nguruwe wa Shilingi Milioni tatu kwa mchezaji wa Simba SC aliyefunga goli pekee la penati katika mchezo wa Simba SC na timu ya Ihefu SC ya mkoani Singida inavyofahamika sasa kama Singida Black Stars iliyotoka sare na Simba SC kwa kufungana bao moja kwa moja.

Amemtaka mchezaji aliyefunga goli la kusawazisha la Simba SC dhidi ya timu ya Ihefu SC, Clatous Chama kufika katika kijiji cha Nguruwe Zamahero Dodoma aweze kukabidhiwa nguruwe mwenye ujauzito ambaye ana thamani ya shilingi Milioni tatu.

No comments:

Powered by Blogger.