LIVE STREAM ADS

Header Ads

Vijana watakiwa kuchangamkia nafasi za kusoma nje ya nchi

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Kaimu Katibu Mtendaji Mkuu wa Tume ya UNESCO Tanzania, Fatuma Mrope (wa kwanza kutoka kulia) akikabidhi cheti kwanufaifaika wa ufadhili wa masomo nchini Poland, George Kato (wa tatu kutoka kushoto) makabidhiano yaliyofanyika Ofisi ya Tume hiyo jijini Dar es Salaam.
***

Vijana nchini wametakiwa kuchangamkia fursa za kusoma nje ya nchi zinazotolewa na Tume ya UNESCO kutoka nchi wafadhili.

Tume ya UNESCO Tanzania imekuwa inapata ufadhili wa vijana katika kusoma nchi mbalimbali lakini changamoto iliyopo ni vijana kutoomba nafasi hizo za kusoma.

Kaimu Katibu Mtendaji Mkuu wa Tume hiyo, Fatuma Mrope amesema nafasi zipo nyingi za kusoma katika nchi za Poland, China na nchi nyingine.

Amesema Teknolojia zinabadilika kila siku katika program za kusoma ambapo nchi ambazo zinatoa ufadhili zimefika mbalimbali ambapo kwenye miradi ya kimkakati inayofanyika nchini wanaweza kutumika kuliko kutafuta nje ya nchi hizo zilizoweza kuwa Teknolojia hizo na zikatoa ufadhili.

Kaimu huyo Fatma amesema kazi ya UNESCO ni kutafuta nchi zenye utayari wa kutoa ufadhili kwa vijana nchi za Afrika katika shahada ya kwanza, Shahada ya pili pamoja na shahada Uzamivu (PhD) na kuzitangaza kwa watanzania ili waweze kuomba na kunufaika nazo.

Akielezea utaratibu ulivyo Afisa Program wa UNESCO Tanzania, Adrian Hyera amesema ufadhili unaotolewa ni bure na kazi kubwa kwa wanahitaji ni kuomba kwenye tovuti za Tume ya Taifa UNESCO Tanzania.

"Nchi nyingi fursa ufadhili wa kusoma wanazitumia zikifika Tanzania vijana hawaombi hadi program za nchi zilitoa ufadhili zinaisha" amesema Hyera.

Aidha amesema kuwa ufadhili huo licha ya kuwa bure ni bure kwa kipindi unachokuwa unasoma na gharama zinazomhusu kama mwanafunzi ni kusoma tu.

Hyera amesema kuwa vijana wanaotaka kupata ufadhili nafasi ziko za kutosha kwani idadi wakati mwingine wanatakiwa 10 nchi lakini Tanzania unakuta hata kijana mmoja hajaenda.

Mmoja wa wanufaika, George Kato aliyekwenda kusoma utalii wa miamba nchini Poland amesema kwa Tanzania alikuwa pekee yake huku baadhi ya nchi zikiwa zina zaidi ya wanafunzi watano.

Kato amesema haoni sababu ya vijana kushindwa kutumia fursa wakati kwao inaongeza utaalam wa kufanya kuingia katika ushindani wa soko la ajira.

Amesema alipoenda ofisi za Tume ya UNESCO Tanzania alipata msaada mkubwa hadi kukamilisha taratibu na kwenda kusoma katika nchi hiyo.

No comments:

Powered by Blogger.