LIVE STREAM ADS

Header Ads

Diwani Gyunda achangia ujenzi wa kanisa la EAGT Maisha Mapya Mwanza

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Diwani wa Viti Maalum CCM Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza, Winfrida Gyunda ameongoza zoezi la ukusanyaji sadaka ya ujenzi katika kanisa la EAGT Maisha Mapya Kaguha lililopo Kata ya Nyamhongolo wilayani humo na kufanikisha kiasi cha shilingi milioni tano kupatikana.

Diwani huo ambaye pia ni mwamini wa kanisa hilo ameongoza zoezi hilo katika ibada iliyofanyika jumapili Aprili 21, 2024 huku akiungwa mkono na familia yake, waumini na marafiki mbalimbali ikiwa ni mara ya pili kufanya hivyo.

Gyunda amesema ujenzi wa jengo la kanisa hilo ambalo ni ghorofa utakamilika kwa utukufu wa Mungu huku akiendelea kuwahimiza waamini wengine wa kanisa hilo kuendelea kuitenda kazi ya hiyo na watazidi kubadirikiwa.

Mchungaji Kanisa la EAGT Maisha Mapya Mwanza, Jonathan Ntibona anasema kila anayeitenda kazi ya Mungu, ataongezewa na kuzidishiwa mahitaji yake.
Na George Binagi- GB Pazzo, BMG
Diwani wa Viti Maalum CCM Wilaya ya Ilemela, Winfrida Gyunda (wa pili kushoto) na familia yake akiongoza zoezi la ukusanyaji sadaka ya ujenzi wa kanisa la EAGT Maisha Mapya Kaguha na kufanikisha kiasi cha shilini milioni tano kupatikana.
Diwani wa Viti Maalum CCM Wilaya ya Ilemela, Winfrida Gyunda (wa nne kushoto) akiongoza zoezi la ukusanyaji sadaka ya ujenzi wa kanisa la EAGT Maisha Mapya Kaguha na kufanikisha kiasi cha shilini milioni tano kupatikana.
Diwani wa Viti Maalum CCM Wilaya ya Ilemela, Winfrida Gyunda (wa pili kushoto) akiwa na familia yake baada ya ibadaya ya jumapili Aprili 21, 2024 iliyoambatana na sadaka ya ujenzi wa kanisa la EAGT Maisha Mapya Kaguha ambapo alifanikisha kiasi cha shilingi milioni tano kupatikana.
Mwonekano wa ujenzi wa jengo la kanisa la EAGT Maisha Mapya Kaguha lililopo Nyamhongolo wilayani Ilemela.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.