LIVE STREAM ADS

Header Ads

Diwani Ilemela aongoza Harambee ya Ujenzi wa Kanisa

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Diwani wa Viti Maalum kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza, Winifrida Gyunda ameongoza harambee ya ujenzi wa Kanisa la EAGT Kaguha Maisha Mapya lililopo Kata ya Nyamhongolo wilayani humo na kufanikisha upatikanaji wa Fedha zaidi ya shilingi milioni tano.

Akizungumza baada ya harambee hiyo iliyofanyika Jumapili Agosti 28, 2022 kanisani hapo, Gyunda ameeleza kufarijika sana baada ya kusaidia upatikanaji wa Fedha zitakazoendeleza ujenzi wa nyumba ya Mungu.

"Leo ilikuwa ni siku ya kusimamia sadaka ya ujenzi kutokana na utaratibu tuliojiwekea kwa sababu kanisa hili halijengwi na wafadhili bali linajengwa na waumimini wenyewe, namshukuru Mungu kwa kuniwezesha kuongoza zoezi hili kwa amani na utulivu" amesema Gyunda ambaye pia ni muumini wa kanisa hilo.

Amesema sadaka inanena mema mbele za Mungu na kwa kuwa ujenzi huo ni mkubwa ametoa wito kwa waumimini kuendelea kujitoa katika kuchangia ili kufika malengo ya kukamilisha nyumba ya Mungu kwa wakati.

Diwani huyo pia ameungwa mkono na familia yake ikiongozwa na mmewe, Amos Mgendi ambaye amesema kupitia harambee hiyo, anaamini Mungu atabariki kazi za mikoa yao na kuimarisha uchumi wa familia.
Kwa upande wake Mchungaji wa kanisa hilo la EAGT Kaguha Maisha Mapya, Jonathan Mathayo amesema makadirio ya ujenzi huo ni shilingi bilioni moja na kwamba matarajio ni kukamilika ifikapo mwaka 2024.

Amesema ushirikiano wa waumini wa kanisa hilo na wadau wengine ndio nguzo pekee itakayowezesha kukamilisha ujenzi huo huku akitumia fursa hiyo kuwaaika watu wote kuwaunga mkono ili kufanikisha ujenzi wa nyumba ya kuabudia.

"Zaburi 133 Bibilia inasema, ndugu wakikaa pamoja kwa umoja Mungu ameamuru baraka juu yao, hivyo naamini japo ujenzi huu ni mkubwa tukikaa pamoja na tukishirikiana mambo yatakwenda vizuri" amesema Mchungaji Mathayo.

Katibu wa Ujenzi wa kanisa hilo, Sarah Paul amesema hadi sasa ujenzi huo uko kwenye hatua za awali na kwamba fedha iliyopatikana kwenye harambee hiyo itasaidia kununua vifaa mbalimbali ambavyo vitaendeleza ujenzi.

Naye John Maziku ambayee ni Mwenyekiti wa Kwaya ya Mwanza Singers kutoka kanisa la EAGT Buzuruga amesema ni vyema waumini wa dini mbalimbali wakawekeza kwenye utoaji ili kuendelea kubarikiwa huku wakijiwekea hazina mbinguni.
Mwonekano wa jengo la kanisa la EAGT Kaguha Maisha Mapya linaloendelea kujengwa.
Diwani wa Viti maalum (CCM) Wilaya ya Ilemela, Winifrida Gyunda (wa pili kulia) akiwa na familia yake wakati wa harambee ya kuchangia ujenzi wa kanisa la EAGT Kaguha Maisha Mapya. Kulia ni Amos Mgendi ambaye ni mme wa Diwani huyo na kushoto ni watoto wao ambapo kwa pamoja wameshiriki kuongoza harambee hiyo.
Diwani wa Viti maalum (CCM) Wilaya ya Ilemela, Winifrida Gyunda akiwa na familia yake (mme na watoto) akiimba wimbo wa kusifu na kuabudu wakati wa harambee ya kuchangia ujenzi wa kanisa la EAGT Kaguha Maisha Mapya.
Mtoto wa Diwani Gyunda (wa pili kushoto) akitoa shukurani baada ya kusimamia harambee hiyo upande wa watoto. Kulia ni baba yao ambaye pia ameshiriki Bega kwa Bega harambee hiyo.
Diwani wa Viti maalum (CCM) Wilaya ya Ilemela, Winifrida Gyunda (kulia) na familia yake wakisimamia harambee ya ujenzi wa kanisa la EAGT Kaguha Maisha Mapya.
Zoezi la harambee likiendelea.
Mwenyekiti wa Kwaya ya Mwanza Singers, John Maziku (wa pili kulia) Akizungumza wakati harambee ya kuchangia ujenzi wa kanisa la EAGT Kaguha Maisha Mapya iliyosumamiwa na Diwani wa Viti Maalum Wilaya ya Ilemela, Winfrida Gyunda (wa tatu kulia) akiwa na familia yake (mme na watoto).
Mchungaji Jonathan Mathayo (kulia) akiiombea familia ya Diwani wa Viti Maalum Wilaya ya Ilemela, Winifrida Gyunda na mmewe Amos Mgendi pamoja na watoto wao baada ya kusimamia zoezi la harambee ya ujenzi wa kanisa la EAGT Kaguha Maisha Mapya. 
Waumini wa kanisa la EAGT Kaguha Maisha Mapya wakiwa kwenye maombi.
Unakaribishwa kuchota Baraka za Mungu kwa kuchangia ujenzi wa kanisa la EAGT Kaguha Maisha Mapya lililopo Nyamhongolo Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza. Wasiliana na Mchungaji wa Kanisa hilo, Jonathan Mathayo kupitia +255 768 11 94 73 ahsante. 
Na Hellen Mtereko, Mwanza

No comments:

Powered by Blogger.