Mama mwenye VVU anaweza kunyonyesha mtoto na asipate maambukizi
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Picha kutoka mtandaoni. |
Moja la tishio kubwa dhidi ya uhai wa mtoto ni kufariki mapema kutokana na kupatwa na maambukizi ya vurusi vya ugonjwa wa upungufu wa kinga mwilini (UKIMWI) kutoka kwa mwama tangu akiwa tumboni.
Kwa mujibu wa wizara ya afya nchini Tanzania, kiwango cha maambukizi wakati wa kunyonyesha kwa mama anayeishi na na Virusi vya Ukimwi (VVU)ni asilimia 5 hadi 10 na hatari ya kijumla bila kunyonyesha ni asilimia 15 hadi 25.
Kwa mujibu wa wizara ya afya hatari ya maambukizi ya VVU kiujumla na kunyoshesha hadi miezi 6 ni ni asilimia 20 hadi 35 hatari ya kijumla na kunyonyesha hadi miezi 18 mpaka 24 ni asilimia 30 hadi 45 na jumla ya hatari ya maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto ni asilimia 20 hadi 40.
Katika kuhakikisha ,ulinzi na usalama wa mtoto tangu akiwa tumboni ,Tanzania imekuwa ikitekeleza Programu jumushi ya taifa ya malezi,makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto inawagusa watoto mwenye umri kati ya miaka 0-8 ikisisistiza juu ya umuhimu wa afya ya mtoto kuanzia mwaka 0-8 ili kuhakikisha mtoto anakua katika utimilifu wake.
Miongoni mwa mambo ambayo program hii inazingatia ni suala la afya ya mtoto kuanzia umri wa mwaka 0-8 ili kuwezesha mtoto kuzaliwa akiwa salama na kukua akiwa salama hasa pale anapozaliwa na mama ambae anaishi na virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Ukimwi.
Kulingana na maelezo ya shirika la afya duniani (WHO), mama mwenye virusi vya UKIMWI kwa nchi zilizo endelea na zenye upatikanaji mzuri wa maji safi na salama anashauriwa kutomnyonyesha mtoto ili kumkinga na uwezekano wa kumuambukiza virusi vya UKIMWI.
Huku kwa nchi maskini na zisizo na upatikanaji mzuri wa maji safi na salama kina mama wanaoishi na VVU wanashauriwa kuwanyonyesha watoto wao huku wakiendelea kupatiwa matibabu ya kufubaza virusi hivyo.
Mtaalamu wa masuala ya VVU na UKIMWI, Bahati Haule.
Mchechemuzi wa masuala ya VVU mkoani Mwanza, Paul Mpazi.
Mchechemuzi wa masuala ya VVU mkoani Mwanza Bwana Paul Mpazi anasema mama ambae ambae amepimwa na kukutwa na maambukizi ya VVU anatakiwa kumnyonyesha mtoto kwa muda wa miezi sita tu ili mtoto asije akapata maambukizi ya VVU kutoka kwa mama.
“Tunasema mwisho miezi sita kwa sababu baada ya hapo mtoto ataota meno hivyo uwezekano wa mtoto kumng’ata mama wakati ananyonya ni mkubwa hivyo kuwa kwenye hatari ya kupata maambukizi”.alisema Paul
Daktari kutoka hospitali ya Mwananchi iliyopo jijini Mwanza Dkt Ezekiel Matabalo anasema ni kweli maziwa ya mama mwenye VVU huwa yamebeba virusi ndani yake lakini mtoto anaweza asipate maambukizi kama mama alikuwa mtumiaji mzuri wa dawa wakati wa ujauzito wake.
Mama anapotumia dawa vizuri pamoja na kufuata taratibu za unyonyeshaji mtoto anakuwa salama kwa sababu kwanza mama anapotumia dawa vizuri inamaana anafubaza virusi kwa kiasi kikubwa na mtoto asipokuwa na michubuko yoyote hawaezi kupata maambukizi.alisema Matabalo.
Kwa upande wake mtaalamu wa masuala ya VVU na UKIMWI Bahati Haule amesema kikubwa anachotakiwa mama mwenye VVU kufanya wakati wa unyonyeshaji ni kutompatia chakula chochote mtoto kwa miezi sita ya unyonyeshaji ili kulinda mtoto na michubuko.
“Tunakataza mtoto asichanganyiwe chochote kwasababu chakula kinaweza kusababisha mchubuko katika utumbo wa mtoto na kupelekea mtoto kupata maambukizi na endapo mama ataona mtoto anamchubuko mdomoni tunashauri akamwone daktari kwa ushauri zaidi” alisema Bhati.
Kutokana na taarifa tofauti tofauti pamoja na takwimu zinazoonyesha hatari ya mtoto kuambukizwa VVU wakati wa unyonyeshaji watu mbalimbali wamekuwa na maswali mengi kuhusu hali hii.
Shekhe wa wilaya ya Magu, Shekhe Mohamed Said.
Shekhe wa wilaya ya Magu Shekhe Mohamed Said anasema amekuwa akisikia wataalamu na vitabu vya dini vikisisitiza mama kunyoshesha mtoto kuanzia mwaka mmoja au na zaidi kwa kadri itakavyompendeza hivyo akataka kujua inakuaje mama mwenye VVU kunyonyesha mtoto mwisho miezi sita.
Kwa upande wake Moses Bundala mwananchi mkazi wa Ukerewe mkoani Mwanza yeye mashaka yake makubwa ni kwenye maziwa ya mama kama yana virusi na inakuaje mtoto anaweza kunyonya maziwa hayo na asipate maambukizi.
Kwa sasa Serikali ya Tanzania kupitia Sera ya Afya 2007 imewekeza katika kuboresha uhai wa mtoto kupitia utoaji wa huduma bure za afya kwa kina mama wajawazito na watoto chini ya miaka 5.
Uwekezaji wa Serikali katika uhai wa mtoto unaonekana dhahiri kwenye kupungua kwa vifo vya watoto kati ya mwaka 2010 na 2015 ambapo kiwango cha vifo vya watoto wachanga (0-28 days) vimepungua kutoka vifo 40 hadi 25 kwa kila vizazi hai 1,000; kiwango cha vifo vyawatoto wachanga (28 days - 11 months) kupungua kutoka vifo 99 hadi 43 kwa kila vizazi hai 1,000; na kiwango cha vifo vya watoto chini ya miaka 5 (12-59 months) vimepungua kutoka vifo 147 hadi 67 kwa kila vizazi hai 1,000. Hii ni kwa mujibu wa sera ya afya 2007.
Programu jumuishi ya melezi,makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto inalenga mtoto mwenye umri wa miaka kuanzia 0-8 huku ikitelekezwa nchi nzima kwa ushiriako kati ya serikali na wadau kutoka asasi zisizo za kiserikali.
Moses Bundala, mkazi wa Ukerewe.
Imeandaliwa na Tonny Alphonce, Mwanza
No comments: