LIVE STREAM ADS

Header Ads

Kampeni ya NMB yatua Kahama

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Wakazi wa Kahama wakifuatilia matukio wakati wa uzinduzi kampeni ya Umebima katika Stendi ya Mabasi ya CDT Mjini Kahama.

Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Benki ya NMB imezindua kampeni ya Umebima Wilaya ya Kahama Mkoa wa Shinyanga - Kanda ya Magharibi kwa lengo la kuhamasisha watanzania kukata bima ili kulinda shughuli zao ikiwemo biashara pindi wanapopatwa na majanga mbalimbali yakiwemo ya moto, mafuriko na ajali zinazoweza kusababisha madhara na kusababisha kuyumba kiuchumi.

Uzinduzi huo uliokwenda sanjari na utoaji elimu na ushauri kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kukata bima umefanyika Jumamosi Aprili 20,2024 katika Kituo cha Mabasi cha CDT Mjini Kahama.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi Seka Urio amesema lengo la Kampeni ya Umebima ni kutoa elimu ya masuala ya bima, kutoa ushauri pamoja na kuuza bima mbalimbali ikiwemo Bima ya Faraja inayolenga zaidi kutoa mafao ya pole kwa mwananchi anapopatwa na changamoto ya msiba au ulemavu ambapo mteja anajiunga kwa Shilingi 200/= na anapata fao kuanzia Sh.milioni 1 hadi 6.
Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi Seka Urio.

“Ndugu zangu hivi karibuni mmekuwa mkishuhudia majanga ya moto, mafuriko na ajali mbalimbali, hivyo ni vyema ukawa na bima ili unapopatwa na majanga usipate hasara na kuepuka kuyumba kiuchumi. Njoo ukate bima kwa ajili yako na mali zako. NMB inashirikiana na kampuni mbalimbali za utoaji bima” amesema Urio.

Kwa upande wake, Meneja Mwandamizi Kitengo cha Bima NMB Makao Makuu, Borondo Chacha amesema Kampeni ya Umebima ni mwendelezo wa kampeni ya Umebima katika Kanda mbalimbali nchini na kwamba wameamua kuzindua Kampeni ya Umebima Wilayani Kahama mkoani Shinyanga katika Kanda ya Magharibi kutokana na kwamba Kahama ni mji unaokua kwa kasi, una mwingiliano mkubwa wa watu lakini pia kuna wateja wengi wa NMB.

“Tunatoa elimu na ushauri kuhusu bima na kuuza bima ili kukabiliana na majanga yanapotokea., tunataka watu wote tuwafikie wapate bima ili kujikinga na hasara zitokanazo na majanga kwa kutoa fidia. Piatuna bima ya maisha, vyombo vya usafiri, bima kwa Wakulima na Wafugaji” amesema Chacha.

Nao baadhi ya wafanyabiashara na wananchi waliofanikiwa kufikiwa na Benki ya NMB na kuwapatia elimu ya bima akiwemo Isaya Kisindo, Baningwa Charles na Moses Masasi wameishukuru Benki ya NMB kwa kupatia elimu ya bima na kuahidi kukata bima ili wao na mali zao ziwe salama na kwamba watahamasisha pia wananchi wengine wakate bima.
Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi Seka Urio akizungumza wakati wa uzinduzi kampeni ya Umebima Wilaya ya Kahama Mkoa wa Shinyanga leo Jumamosi Aprili 20,2024 katika Stendi ya Mabasi CDT Mjini Kahama.
Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi Seka Urio akizungumza wakati wa uzinduzi kampeni ya Umebima Wilaya ya Kahama Mkoa wa Shinyanga.
Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi Seka Urio akizungumza wakati wa uzinduzi kampeni ya Umebima Wilaya ya Kahama Mkoa wa Shinyanga.
Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Kahama, Said Pharseko akizungumza wakati wa uzinduzi kampeni ya Umebima Wilaya ya Kahama Mkoa wa Shinyanga.
Wafanyakazi wa Benki ya NMB wakipiga picha ya kumbukumbu wakati wa uzinduzi kampeni ya Umebima Wilaya ya Kahama Mkoa wa Shinyanga
Wafanyakazi wa Benki ya NMB wakipiga picha ya kumbukumbu wakati wa uzinduzi kampeni ya Umebima Wilaya ya Kahama Mkoa wa Shinyanga.
Mabango wakati wa uzinduzi kampeni ya Umebima.
Mabango wakati wa uzinduzi kampeni ya Umebima.
Mabango wakati wa uzinduzi kampeni ya Umebima.
Wakazi wa Kahama wakifuatilia matukio wakati wa uzinduzi kampeni ya Umebima katika Stendi ya Mabasi ya CDT Mjini Kahama.
Wakazi wa Kahama wakifuatilia matukio wakati wa uzinduzi kampeni ya Umebima katika Stendi ya Mabasi ya CDT Mjini Kahama.
Wakazi wa Kahama wakifuatilia matukio wakati wa uzinduzi kampeni ya Umebima katika Stendi ya Mabasi ya CDT Mjini Kahama.
Burudani ikiendelea wakati wa uzinduzi kampeni ya Umebima katika Stendi ya Mabasi ya CDT Mjini Kahama.
Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi Seka Urio (kushoto) akitoa elimu ya bima kwa mfanyabiashara Moses Masasi wakati wa uzinduzi kampeni ya Umebima Wilaya ya Kahama Mkoa wa Shinyanga.
Mfanyabiashara Moses Masasi akihamasisha wananchi kukata bima wakati wa uzinduzi kampeni ya Umebima Wilaya ya Kahama Mkoa wa Shinyanga.
Meneja Mwandamizi Kitengo cha Bima NMB Makao Makuu, Borondo Chacha akitoa elimu ya bima kwa mfanyabiashara Moses Masasi wakati wa uzinduzi kampeni ya Umebima Wilaya ya Kahama Mkoa wa Shinyanga.
Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi Seka Urio (kushoto) akitoa elimu ya bima kwa mfanyabiashara Isaya Kisindo wakati wa uzinduzi kampeni ya Umebima Wilaya ya Kahama Mkoa wa Shinyanga.
Meneja Mwandamizi Kitengo cha Bima NMB Makao Makuu, Borondo Chacha (kushoto) akitoa elimu ya bima kwa mfanyabiashara Isaya Kisindo wakati wa uzinduzi kampeni ya Umebima Wilaya ya Kahama Mkoa wa Shinyanga.
Mfanyabiashara Borondo Chacha akiishukuru na kuipongeza Benki ya NMB kutoa elimu kwa wananchi kwani wengi hawajui faida ya bima.
Meneja Mwandamizi Kitengo cha Bima NMB Makao Makuu, Borondo Chacha akitoa elimu ya bima kwa mfanyabiashara Baningwa Charles wakati wa uzinduzi kampeni ya Umebima Wilaya ya Kahama Mkoa wa Shinyanga.
Meneja Mwandamizi Kitengo cha Bima NMB Makao Makuu, Borondo Chacha akizungumza wakati wa uzinduzi kampeni ya Umebima Wilaya ya Kahama Mkoa wa Shinyanga.
Viongozi wa Benki ya NMB wakipita mtaa kwa mtaa Mjini Kahama kutoa elimu na ushauri kuhusu Bima wakati wa uzinduzi kampeni ya Umebima Wilaya ya Kahama Mkoa wa Shinyanga.

Muonekano sehemu ya eneo la uzinduzi kampeni ya Umebima Wilaya ya Kahama Mkoa wa Shinyanga.
Muonekano sehemu ya eneo la uzinduzi kampeni ya Umebima Wilaya ya Kahama Mkoa wa Shinyanga.
Muonekano sehemu ya eneo la uzinduzi kampeni ya Umebima Wilaya ya Kahama Mkoa wa Shinyanga.

No comments:

Powered by Blogger.