Michuano ya 'Tigo Chuo Challenge Cup 2024' yaanza Mwanza
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Michuano ya vyuo vya kati na vyuo vikuu ya 'Tigo Chuo Challenge Cup 2024' imeanza kutimia katika uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza.
Michuano hiyo imeanza Jumamosi Aprili 27, 2024 ikiwa ni msimu wa tatu ambapo mechi ya kwanza, chuo cha Mipango kimeibuka na ushindi wa goli 2:1 dhidi ya chuo cha MacWish huku mchezo wa pili kati ya chuo cha GEMA ukimalizika kwa sare tasa (0:0) dhidi ya chuo cha Kolandoto.
Akizungumza wakati wa michuano hiyo, Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Ziwa, Joseph Mutalemwa alisema michezo ni afya na ajira kwa vijana hivyo kampuni hiyo inaipa umuhimu kama ilivyo kipaumbele kwa Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na ndiyo maana imehamasisha kudhamini michuano hiyo.
Mratibu wa michuano hiyo, Dickson Mpilipili alisema michuano hiyo ni fursa ya kuibua vipaji vya soka kwa vijana ambapo misimu miwili iliyopita iliibua wachezaji ambao sasa wanacheza katika ligi tofauti tofauti akiwemo mmoja anayecheza Biashara United na Polisi Tanzania na kwamba msimu huu fainali ya michuano hiyo inayoshirikisha vyuo 16 itapigwa Mei 18,2024.
Awali akifungua michuano hiyo, Afisa Elimu Mkoa Mwanza Mwl. Martin Nkwabi aliipongeza kampuni ya Tigo kwa kudhamini michuano hiyo na rai kutoa rai kushuka zaidi hadi ngapi ya shule za msingi na sekondari ili kuibua zaidi vipaji vya watoto na kuvikuza.
Nao baadhi ya wanafunzi wa vyuo vinavyoshiriki michuano hiyo walimiza wadau wa michezo kama Tigo kuendelea kushirikiana na Serikali kuboresha miundombinu ya michezo ikiwemo viwanja, kusaidia upatikanaji wa zana za michezo kama mipira na sare ili hatua itakayoongeza chachu ya kuibua vipaji zaidi kwa wanafunzi huku wakiendelea kujiweka imara kiafya kupitia michezo.
Msimu wa kwanza Chuo Challenge Cup bingwa alikuwa chuo cha SAUT, msimu wa pili chuo cha Kaliua ambapo msimu wa tatu bingwa anatarajiwa kujulikana Mei 18, 2024.
Na George Binagi- GB Pazzo, BMG
Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Ziwa, Joseph Mutalemwa akizungumza na waandishi wa habari katika uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza wakati wa ufunguzi wa michuano ya mpira wa miguu ya Tigo Chuo Challenge Cup 2024. Kulia ni Meneja Masoko wa Tigo Kanda ya Ziwa, Mussa Mwakapala.
Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Ziwa, Joseph Mutalemwa akizungumza wakati wa ufunguzi wa michuano ya Tigo Chuo Challenge Cup 2024 jijini Mwanza.
Afisa Elimu Mkoa wa Mwanza, Mwl. Martin Nkwabi akizungumza na waandishi wa habari wakati akifungua michuano ya mpira wa miguu ya Tigo Chuo Challenge Cup 2024 katika dimba la Nyamagana jijini Mwanza. Kushoto ni Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Ziwa, Joseph Mutalemwa.
Mchezaji wa timu ya Mipango (kushoto) akiondoa mpira katika eneo la hatari wakati wa mchezo dhidi ya timu ya MacWish.
Tazama BMG TV hapa chini
PIA>>> BONYEZA HAPA KUSOMA ZAIDI
No comments: