LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mbunge wa Nyamagana aguswa na adha ya barabara za mitaa

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Mbunge wa Jimbo la Nyamagana mkoani Mwanza, Stanslaus Mabula ameguswa na changamoto ya uharibifu wa baadhi ya barabara za mitaa katika jimbo hilo na kukabidhi mifuko ya simenti ili kusaidia ukarabati wake.

Akizungumza Jumapili Mei 26, 2024 wakati wa kukabidhi mifuko 210 ya simenti kwa ajili ya ukarabati wa barabara ya Mtaa wa SDA Kata ya Isamilo, Mabula alisema mpango uliopo ni kuhakikisha barabara korofi za mitaa zinapitika ili kuwaondolea adha wananchi.

"Niendelee kumshukuru Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutuletea fedha kupitia mfuko wa jimbo ambazo zimetusaidia kuleta mifuko ya simenti ili kuwaunga mkono wananchi katika ukarabati wa barabara hii" alisema Mabula akisema ataendelea kufuatilia barabara korofi ili kuhakikisha zinapitika.

Mabula alisema jimbo la Nyamagana lina zaidi ya km 1,000 za barabara za mitaa, lakini zinazopitika vizuri kwa sasa hazifiki km 200 ataendelea kuishinikiza Serikali kuendelea kutoa fedha ili kufanyia marekebisho barabara hizo huku akiwapongeza wakazi wa Mtaa wa SDA kwa kuchukua hatua ya kuanza ujenzi wa barabara katika Mtaa huo.

Naye Diwani wa Kata ya Isamilo, Charles Nyamasiriri alisema kwa kushirikiana na wananchi walianzisha ujenzi wa barabara ya Mtaa wa SDA yenye urefu wa Mita 500 hivyo amempongeza Mbunge Mabula kwa kuunga mkono juhudi hizo.
Na George Binagi- GB Pazzo, BMG 
Mbunge wa Jimbo la Nyamagana mkoani Mwanza, Stanslaus Mabula (mwenye kofia) akikabidhi mifuko ya simenti kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya Mtaa wa SDA Kata ya Isamilo inayojengwa kwa kiwango cha zege.
Mbunge wa Jimbo la Nyamagana mkoani Mwanza, Stanslaus Mabula (mwenye kofia) akizungumza na wakazi wa Mtaa wa SDA baada ya kukabidhi mifuko ya simenti.
Mbunge wa Jimbo la Nyamagana mkoani Mwanza, Stanslaus Mabula (mwenye kofia) akizungumza na wakazi wa Mtaa wa SDA baada ya kukabidhi mifuko ya simenti kwa ajili ya ujenzi wa barabara kwa kiwango cha zege.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo Mtaa wa SDA Kata ya Isamilo akitoa shukurani kwa Mbunge Stanslaus Mabula kwa kuwaunga mkono kwenye ujenzi wa barabara.
Wakazi wa Mtaa wa SDA Kata ya Isamilo wakiwa kwenye mapokezi ua mifuko ya simenti iliyotolewa na Mbunge wao Stanslaus Mabula.
Mbunge wa Jimbo la Nyamagana mkoani Mwanza, Stanslaus Mabula amekabidhi mifuko 210 ya simenti katika Mtaa wa SDA na kuahidi mifuko 60 Mtaa jirani wa Nyakabungo kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya mtaa kwa kiwango cha zege.
Mbunge wa Jimbo la Nyamagana mkoani Mwanza, Stanslaus Mabula (kulia) akipokea pongezi kutoka kwa wakazi wa Mtaa wa SDA Kata ya Isamilo baada ya kukabidhi mifuko 210 ya simenti kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya mtaa kwa kiwango cha zege.
Wakazi wa Mtaa wa SDA wakimsikiliza Mbunge wao, Stanslaus Mabula.
Mbunge wa Jimbo la Nyamagana mkoani Mwanza, Stanslaus Mabula akizungumza na wakazi wa Mtaa wa SDA wakati wa kukabidhi mifuko ya simenti.
Mifuko 210 ya simenti iliyokabidhiwa na mbunge Stanslaus Mabula katika Mtaa wa SDA Kata ya Isamilo jijini Mwanza.
Wakazi wa Mtaa wa SDA wakimsikiliza Mbunge wa Jimbo la Nyamagana mkoani Mwanza, Stanslaus Mabula
Katibu Mwenezi wa CCM akimpongeza mbunge Stanslaus Mabula kwa kukabidhi mifuko ya simenti katika Mtaa wa SDA.
Diwani wa Kata ya Isamilo, Charles Nyamasiriri (kulia) akizungumza wakati wa kupokea mifuko 210 ya simenti katika Mtaa wa SDA.
Zoezi la kushusha mifuko ya simenti katika Mtaa wa SDA Kata ya Isamilo jijini Mwanza.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.