LIVE STREAM ADS

Header Ads

Watanzania wazidi kuchangamkia uwekezaji nguruwe

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Msanii wa sanaa ya uchekeshaji chini maarufu kam Mr. Mwanya ametembelea Kijiji cha Nguruwe kilichopo Zamahero jijini Dodoma kwa ajili ya kujionea uwekezaji mkubwa unaofanywa na Mkurugenzi wa Kijiji cha Nguruwe Project Simon Mkondya Maarufu kama Mr. Manguruwe.

Msanii huyo pia ameweka wazi juu ya uwekezaji alioufanya katika eneo hilo ambapo amesema mara tu alipobahatika kufahamu habari kutoka katika kijiji hicho cha nguruwe amefanya uwekezaji mkubwa.

Akiwa katika kijiji hicho Mr. Mwanya ameonesha kufurahishwa na uwekezaji alioufanya kwani umeshaanza kumpa faida kubwa ya uwekezaji wake.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mr. Mwanya amesema kama watanzania hususani vijana wataamka na kuanza kufanya uwekezaji huu katika kijiji hicho cha nguruwe, changamoto ya kulalamika juu ya ukosefu wa ajira itapungua.

Mkurugenzi wa kijiji hicho, Simon Mkondya ameipongeza Serikali kwa kuendelea kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji na kusema itasaidia kuongeza wawekezaji wa ndani na hivyo kuwataka watanzania hususani vijana kuchangamkia fursa ya uwekezaji wa nguruwe.
Msanii, Mr. Mwanya akiwa katika Kijiji cha Nguruwe kilichopo Zamahe Dodoma.
Mkurugenzi wa mradi wa Kijiji cha Nguruwe, Simon Mkondya.

No comments:

Powered by Blogger.