LIVE STREAM ADS

Header Ads

Timu ya Pamba Jiji FC yapata mapokezi makubwa Mwanza

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Timu ya soka ya Pamba Jiji imepata mapokezi makubwa kutoka kwa mashabiki na viongozi mbalimbali mkoani Mwanza, baada ya kufanikiwa kurejea Ligi Kuu yaTanzania Bara msimu wa mwaka 2024/25.

Mapokezi ya timu hiyo yamefanyika Jumanne Aprili 30, 2024 kuanzia eneo la Hungumalwa wilayani Kwimba na kupita mitaa mbalimbali ya Misungwi, Ilemela na hatimaye uwanja mkongwe wa Nyamagana jijini Mwanza.

Mapokezi hayo yameongozwa na Mkuu wa Mkoa Mwanza, Said Mtaka aliyekuwa bega kwa bega na timu hiyo tangu alipohamishiwa mkoani Mwanza akitokea mkoani Mara, timu ya Pamba ikiwa imebakiza mechi nne zilizotoa maamuzi ya kurejea Ligi Kuu ikiwemo mechi ya mwisho iliyochezwa ugenini Aprili 28, 2024 ambapo Pamba Jiji iliibuka na ushindi wa goli tatu kwa moja dhidi ya Mbuni.

Akizungumza kwenye mapokezi hayo, Mtanda ametambua mchango wa wachezaji, wadau na viongozi mbalimbali waliofanikisha timu ya Pamba Jiji FC kurejea ligi kuu akiwemo aliyekuwa Mkuu wa Mkoa Mwanza, Amos Makalla ambaye sasa ni Katibu Mwenezi, Itikadi na Mafunzo CCM.

“Nyamagana utakuwa uwanja wa nyumbani wa Pamba Jiji, nimwelekeze Mkurugenzi kuja na mpango wa kuongeza majukwaa katika uwanja huu na jukwaa moja liitwe Amos Makalla ili kumuenzi kwa vitendo” alisema Mtanda na kuongeza kuwa uwanja wa Nyamagana utafanyiwa maboresho na kuwekewa taa ili kutoa fursa michezo kufanyika usiku.

Pia Mtanda alitambua mchango wa wachezaji wa zamani wa Pamba akiwemo Khalid Bitebo Zembwela aliyewezesha timu hiyo kutwaa ubingwa wa ligi kuu mwaka 1990 ikiivua ubingwa Malindi ya Zanzibar ambayo ilitwaa ubingwa mwaka 1989 kwa kuifunga Pamba kwa mkwaju wa penati.

“Leo nitamkaidhi Zembwela zawadi ya shilingi milioni moja kwa mchango wake, lakini pia ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mwanza inaahidi kuwakatia bima ya afya wachezaji walioanzisha timu ya Pamba ili waendelee kufurahia maisha baada ya kustaafu” alisema Mtanda na kuongeza kuwa wachezaji hao wataandaliwa kadi maalumu ya kuingia uwanjani kushuhudia bure michezo ya Pamba Jiji FC.

Mtanda alisema mikakati iliyopo kwa Pamba Jiji FC iliyoanzishwa mwaka 1984 na kuondoshwa kwenye michuano ya ligi kuu mwaka 2001 ni kushirikiana na wadau kununua basi la kisasa kwa ajili ya wachezaji na kujenga ‘hostel’ za kisasa ili timu ikae eneo lenye hadhi inayoendana na Jiji la Mwanza.

Katika hatua nyingine Mtanda atashirikiana na Makalla pamoja na viongozi mkoani Mara ili kuhakikisha timu ya Biashara United inayocheza hatua ya ‘play off’ nayo inarejea ligi kuu akisema nayo ni timu ya Kanda ya Ziwa hivyo ni vyema timu zote zikafanya vizuri katika michezo ingawa aliweka wazi kuwa viongozi wa kisiasa hawataingia masuala ya uongozi wa timu hizo bali watasalia kuwa washauri na timu zitaendeshwa na viongozi wake.

Timu ya soka ya Pamba Jiji FC ikiongozwa na kocha Mbwana Makata na nahodha Jerry Tegete imeahidi kufanya vizuri baada ya kurejea ligi kuu soka Tanzania Bara kwani kila eneo walilopita kwenye mapokezi, msisitizo wa mashabiti uliwataka wasishuke tena daraja.
Na George Binagi- GB Pazzo, BMG
Mkuu wa Mkoa Mwanza, Said Mtanda (kushoto) na viongozi mbalimbali mkoani Mwanza akiwemo Mwenyekiti wa chama cha soka Mkoa Mwanza, Vedastus Lufano (katikati) wakiwapokea wachezaji na viongozi wa timu ya Pamba Jiji FC kwenye mapokezi yaliyofanyika uwanja wa Nyamagana.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, Said Mtanda akizungumza kwenye mapokezi ya timu ya Pamba Jiji FC baada ya kurejea ligi kuu soka Tanzania Bara.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, Said Mtanda akimpongeza mchezaji wa zamani wa timu ya Pamba, Khalid Zembwela (kushoto) aliyeiwezesha timu hiyo kutwaa ubingwa wa Tanzania mwaka 1990.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, Said Mtanda (kulia) akikabidhi ngao kwa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa Mwanza, Amos Makalla (hayuko pichani) kama sehemu ya kutambua mchango wake wa kufanikisha Pamba Jiji FC kurejea ligi kuu. Ngao hiyo imepokelewa kwa niaba yake na Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza, Sima Costantine (kushoto).
Mkuu wa Mkoa Mwanza, Said Mtanda (kushoto) akikabidhi cheti cha pongezi kwa Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza, Simba Costantine kwa mchango wake wa kuiwezesha timu ya Pamba Jiji FM kurejea ligi kuu soka Tanzania Bara msimu wa 2024/25.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, Said Mtanda (kushoto) akikabidhi cheti cha pongezi kwa Naibu Meya wa Jiji la Mwanza, Bhiku Kotecha kwa mchango wake wa kuiwezesha timu ya Pamba Jiji FM kurejea ligi kuu soka Tanzania Bara msimu wa 2024/25.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, Said Mtanda (kushoto) akikabidhi cheti cha pongezi kwa Mbunge wa Jimbo la Nyamagana, Stanslaus Mabula (kulia) kwa mchango wake wa kuiwezesha timu ya Pamba Jiji FM kurejea ligi kuu soka Tanzania Bara msimu wa 2024/25.
MNEC Christopher Mwita Gachuma akipokea cheki cha pongezi kwa mchango wake wa kuisaidia timu ya Pamba Jiji FC kurejea ligi kuu.
Mwakilishi wa kampuni ya Net Sports akipokea cheti cha pongezi kwa kuisadia timu ya Pamba Jiji FC kurejea ligi kuu.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, Said Mtanda (kushoto) akikabidhi cheti cha pongezi kwa mdau wa soka kwa mchango wake wa kuiwezesha timu ya Pamba Jiji FM kurejea ligi kuu soka Tanzania Bara msimu wa 2024/25.
Kocha Mkuu wa timu ya Pamba Jiji FC, Mbwana Makata akionyesha cheti cha pongezi baada ya kufanikiwa kuirejesha ligi kuu timu hiyo.
Viongozi mbalimbali wa timu ya Pamba wakiwa na vyeti vya pongezi.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, Said Mtanda akiwa na viongozi mbalimbali wakifurahia mapokezi ya timu ya Pamba Jiji FC.
Viongozi mbalimbali jukwaa kuu wakiwa kwenye mapokezi ya timu ya Pamba Jiji FC akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe, Christopher Ngubiagai (katikati).
Viongozi mbalimbali jukwaa kuu wakiwa kwenye mapokezi ya timu ya Pamba Jiji FC akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe, Christopher Ngubiagai (katikati).
Viongozi mbalimbali jukwaa kuu wakiwemo wakuu wa Wilaya za Ilemela, Misungwi na Ukerewe wakiwa kwenye mapokezi ya timu ya Pamba Jiji FC akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe, Christopher Ngubiagai (katikati).
Mashabiki wa timu ya Pamba Jiji FC wakiwa kwenye mapokezi hayo ambayo yalianzia Kwimba, Misungwi na kuingia jijini Mwanza kupitia barabara ya Buhongwa, Pamba, Buzuruga, Nyasaka, Pasiansi, mjini kati na kuhitimishwa uwanja wa Nyamagana.
Viongozi mbalimbali jukwaa kuu.
Tazama BMG TV hapa chini
PIA SOMA>>> Habari zaidi hapa

No comments:

Powered by Blogger.