Maadhimisho ya siku ya kutokomeza utumikishwaji wa watoto yafanyika Simiyu
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Tanzania imeungana na mataifa mbalimbali duniani kuadhimisha siku ya kupinga utumikishwaji na ajira hatarishi kwa watoto ambayo kitaifa imefanyika katika stendi ya Mwanhuzi, Wilaya ya Meatu mkoani Simiyu.
Maadhimisho hayo yamefanyika Jumatano Juni 12, 2024 ambapo mgeni rasmi Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu- Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu, Patrobas Katambi amezindua awamu ya pili ya mkakati wa kitaifa wa kutokomeza utumikishwaji watoto utakaotekelezwa kwa kipindi cha mwaka 2024/25 hadi 2028/29.
Viongozi wa Serikali, wananchi na mtandao wa mashirika yanayopinga utumikishwaji na ajira hatarishi kwa watoto Tanzania (TCACL), wameshiriki maadhimisho hayo na kutoa rai kuunganisha nguvu ya pamoja ili kuwaokoa mamilioni ya watoto wanaotumikishwa katika kazi hatarishi ikiwemo migodini, mashambani, viwandani na majumbani.
Miongoni mwa mashirika yaliyoshiriki maadhimisho hayo ni shirika la kutetea haki za wafanyakazi wa nyumbani (WoteSawa) la jijini Mwanza ambalo kwa kipindi cha mwaka 2018/24 limefanikiwa kuwaokoa watoto 130 kutoka kwenye ajira hatarishi na utumikishwaji.
Tazama BMG TV hapa chini
PIA>>> BONYEZA HAPA KUSOMA ZAIDI
No comments: