Wadau sekta ya habari na mawasiliano wajadiliana kanuni za maudhui ya mtandaoni
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Mkurugenzi wa MISA-TAN Elizaberth Riziki.
Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini Mwa Afrika Tawi la Tanzania (MISA-TAN) kwa kushirikiana na Protection International Africa (PIA) wamefanya Warsha na Wadau Sekta ya Habari na Mawasiliano, kujadili na kutoa maoni juu ya Kanuni za Maudhui ya Mtandaoni ya mwaka 2018.
Warsha hiyo imefanyika Juni 26, 2024 Jijini Dar es salaam kwa ufadhili wa ubalozi wa Finland nchini Tanzania.
Akizungumza kwenye Warsha hiyo Mkurugenzi wa MISA-TAN Elizaberth Riziki, amesema wamekuwa wakiendesha Warsha za namna hiyo ili kujadili Sheria mbalimbali za habari, ambapo mwaka jana walikuwa pia na Mjadala wa Sheria ya huduma za habari ya mwaka 2016, na mwaka huu wanajadili kuhusu Kanuni za Maudhui ya Mtandaoni ya mwaka 2018 na maboresho yake.
Amesema katika Mjadala huo wa Kanuni za Maudhui ya Mtandaoni 2018 utaibua mambo mengi, sababu wadau watajadili Kanuni hizo na kutoa maoni yao mbalimbali zikiwamo changamoto za sharia hiyo.
“Tunaishukuru Serikali kwa kuonyesha nia ya kubadilisha Kanuni za Habari, usiposhukuru kwa madogo huwezi kupewa makubwa,huu Mradi ambao tunafanya na Ubalozi wa Finland na Protection Africa tunataka kuongeza uelewa juu ya Kanuni ya Maudhui ya Mtandaoni ya mwaka 2018, kama tulivofanya mwaka jana kwenye Sheria ya huduma ya habari ya mwaka 2016” amesema Riziki.
Mwezeshaji kwenye wa warsha hiyo, Deus Kibamba amesema kanuni za maudhui ya mtandaoni za mwaka 2018 zilitungwa ili kudhibiti uholela wa kusambaza taarifa mtandaoni.
“Tunapojadili Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta EPOCA (2010) inampa Waziri wa Sekta husika kutunga Kanuni itakayo ruhusu na kudhibu maudhui ya Mtandaoni, na Kanuni hizi zilitungwa mwaka 2018 ” amesema Kibamba.
Amesema wadau wa habari na qaandishi wa habari, wanapaswa kuzijua kanuni hizo za maudhui ya mtandaoni na kuzitekeleza wakati wa kusambaza taarifa ili kujiweka salama.
Ametolewa mfano Kanuni ya 3 inayosema hata kupokea maudhui ambayo yapo kwenye utata na ukayasambaza ni kosa, na hata kutumia mtandao wako kuchukua maudhui hayo napo upo kwenye hatari, jambo ambalo hufanywa na watu wengi katika kusambaza taarifa.
Kibamba amezungumzia pia kwa upande wa utoaji wa lesseni za muadhui ya mtandaoni, kwamba kumekuwa na masharti mengi ambayo yamekuwa yakisababisha upatikanaji wa leseni kuwa mgumu.
“Kanuni hii ya Maudhui Mtandaoni ya mwaka 2018 ili kuja kudhibiti uholela wa kusambaza taarifa Mtandaoni,hata leseni zake zinaisha baada ya miaka mitatu, na kama maudhui yako yalikuwa na shida siku ukienda kuhuisha leseni yako unabanwa na huenda usipewe, lakini Leseni za NGO zenyewe huisha muda wa miaka 10, hivyo leseni yako ikiwa ya muda mfupi ina maana hakuna uaminifu” amesema Kibamba.
Naye Wakili Gideoni Mandes akizungumza kwenye warsha hiyo, ameishauri Serikali kuona uwezekano wa kupunguza ada ya usajili vyombo vya habari vya mtandaoni ili ziwe rafiki na kuwezesha hata vijana ambao wanatoka vyuo wapate kuzimudu na kujiajiri.
Patrick Kipangula kutoka Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali, amesema suala ya upunguzaji wa Ada za Usajili za Media za Mtandaoni tayari lipo kwenye mchakato wa kufanyiwa kazi.
Na Marco Maduhu, Dar
Mkurugenzi wa MISA-TAN, Elizaberth Riziki.
Mbobezi wa masuala ya sheria, Deus Kibamba.
Wakili Gideoni Mandes.
Afisa Program kutoka LHRC, Raymond Kanegel.
Patrick Kipangula kutoka Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali.
Picha ya Pamoja.
No comments: