LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mbunge Kishapu aunga mkono utekelezaji wa miradi ya maendeleo

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Mbunge wa Jimbo la Kishapu mkoani Shinyanga, Boniphace Butondo amekabidhi mifuko ya saruji 1,012 na mabati 456 vyote vikiwa na thamani ya shilingi 86,000,000 katika Kata 17.

Akikabidhi vifaa hivyo Julai 11,2024 katika Hospitali ya Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete wilayani Kishapu, Butondo alisema ni utaratibu wa Serikali kutoa fedha kwenye mfuko wa jimbo kutokana na ukubwa wa eneo na idadi ya watu hivyo walipokea kiasi cha Shilingi 86,000,000 hivyo ametoa vifaa hivyo kulingana na mahitaji ya kila Kata jimboni humo.


Vifaa hivyo vimekabidhiwa katika Kata za Mwataga, Ndololeji, Shagihilu, Idukilo, Mwakipoya, Talaga,Ngofila, Itilima, Mwamalasa, Bubiki, Kiloleli, Mwasubi, Sekebugolo, Masanga, Kishapu, Mondo na Igaga kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ikiwemo elimu na afya.
Mbunge wa Jimbo la Kishapu mkoani Shinyanga, Boniphace Butondo (kushoto) akikabidhi vifaa vya ujenzi katika Kata za Jimbo hilo.
Msaada wa simenti uliotolewa na mbunge wa Kishapu.
Baadhi ya mifuko ya simenti iliyotolewa katika jimbo la Kishapu.
Na Sumai Salum, Kishapu

No comments:

Powered by Blogger.