Watuhumiwa 179 watiwa mbaroni Mwanza
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Wilbroad Mutafungwa.
Na Chausiku Said, Mwanza
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza linawashikilia watu 179 kwa tuhuma mbalimbali akiwemo Lupande Paschal (43) mkazi wa Kijiji cha Kasele wilayani Sengerema anayetuhumiwa kuhusika na mauaji ya Mwajuma Yugele kwa kumpiga na kitu kizito kichwani.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Wilbrod Mutafungwa amesema chanzo cha tukio hilo la mauji ni wivu wa kimapenzi.
Mtafungwa ameeleza kuwa baada ya kupata taarifa hiyo ya mauji, walifanya upelelezi na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo akiwa amejificha katika Kijiji cha Busango Kata ya Segese Wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga.
Aidha Mutafungwa ameongeza kuwa kwa kipindi cha mwezi mmoja iliopita, wamefanya operesheni dhidi ya waharifu na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa 179 kwa kuhusika na tuhuma mbalimbali
Mtafungwa ameeleza kuwa watuhumiwa 39 waliokamatwa walikuwa dawa za kulevya aina ya bangi KG 14.2, 63 wakiwa na lita 134.5 za pombe haramu ya moshi (gongo) na mitambo mitano ya kutengeneza pombe hiyo.
Wengine 63 wakiwa na vifaa vya kupigia ramli chonganishi na wawili wakiwa na 'injector pump' ambao ni mtambo unaotumika kutengenezea barabara huku vielelezo mbalimbali ikiwemo deki za runinga, pikipiki aina ya TVS, Sunlg, Bajaji na Kinglion zinazodhaniwa kuwa za wizi.
No comments: