LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mhubiri wa kimataifa kutoka Kenya aandaa mkutano mkubwa Mwanza

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Mhubiri wa kimataifa kutoka nchini Mombasa nchini Kenya, mchungaji Ezekiel Odero wa kanisa la 'New Life Prayer Centre' anatarajiwa kufanya mkutano mkubwa katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza kuanzia Julai 24-28, 2024.

Akizungumza na waandishi wa habari Jumanne Julai 16, 2024 baada ya kuwasili jijini Mwanza kukagua maandalizi ya mkutano huo, mchungaji Odero alisema licha ya watu wengi kufunguliwa kwenye mikutano yake laki bado amekuwa akiwahimiza kutopuuza huduma za afya zinatolewa na wataalamu wa afya.

"Mtoto wangu watu watatu wote wamezaliwa hospitalini, pia mke wangu alifanyiwa upasuaji wakati wa kujifungua ambapo madaktari walinisaidia sana, wasingekuwepo labda tungekuwa tunaongea historia nyingine" alisema Mchungaji huyo huku akiwahimiza viongozi wengine wa dini kutowazuia waumini wao kupata huduma za afya hospitalini kwa kutegemea maombi pekee.

Pia mchungaji Ezekiel aliwataka wakazi wa Jiji la Mwanza kujitokeza kwa wingi katika mkutano huo wa injili ili kujionea namna Mwenyezi Mungu atakavyotenda miujiza kwa kuwafungua wenye mahitaji mbalimbali.

Awali Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Said Mtanda alisema atahakikisha wataalamu wa afya wanakuwepo kwenye mkutano huo ili kutoa huduma mbalimbali za afya pindi zitakapohitajika.

Naye Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza, Wilbroad Mutafungwa alisema jeshi hilo litaimarisha ulinzi na usalama wakati wote wa mkuano huo ambapo tayari mikutano ya aina hiyo hapa nchini imefanyika Arusha, Dar es salaam na Morogoro. 
Mhubiri wa kimataifa kutoka nchini Mombasa nchini Kenya, mchungaji Ezekiel Odero wa kanisa la New Life akiwasili jijini Mwanza kwa ajili ya maandalizi ya mkutano wake wa injili.
Mhubiri wa kimataifa kutoka nchini Mombasa nchini Kenya, mchungaji Ezekiel Odero wa kanisa la New Life (wa tatu kulia) akikagua uwanja wa CCM Kirumba.
Mhubiri wa kimataifa kutoka nchini Mombasa nchini Kenya, mchungaji Ezekiel Odero wa kanisa la New Life na waumini wake wakiombea ardhi ya Jiji la Mwanza kuelekea mkutano wa injili utakaofanyika Julai 24-28, 2024.
Mhubiri wa kimataifa kutoka nchini Mombasa nchini Kenya, mchungaji Ezekiel Odero wa kanisa la New Life akiombea na kubariki ardhi ya Jiji la Mwanza kuelekea kwenye mkutano wake utakaoanza Julai 24-28, 2024.

Itakumbukwa Aprili 27, 2023 mchungaji Odero aligonga vichwa vya habari baada ya kukamatwa na polisi nchini Kenya kwa mahojiano na kisha kuachiwa kufuatia miili iliyofichuliwa ikiwa imefukiwa katika msitu wa Shakahola Kaunti ya Kilifi nchini Kenya.

Miili hiyo iliaminiwa kuwa ya waumini wa kanisa la 'Good News International' linaloongozwa na mchungaji Paul Mackenzie ambaye hadi sasa anashikiliwa na polisi ambapo ilidaiwa wawili hao awali walikuwa na ushirika wa ukaribu.
Na Chausiku Said Mwanza 

No comments:

Powered by Blogger.