LIVE STREAM ADS

Header Ads

Shilole apata ubalozi

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Msanii na Mama lishe Zuwena Mohamed maarufu kama Shilole (Shishifood) ametangazwa kuwa balozi mpya wa kampuni ya Gesi ya Oryx kwa ajili ya kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia kupitia mitungi ya gesi nchini.

Lengo la Oryx kumpa ubalozi Shilole ni kuunga mkono juhudi za Rais Dk.Samia Suluhu ambaye ameweka malengo kuwa ifikapo mwaka 2032 asilimia 80 ya Watanzania iwe inatuminia nishati safi ya kupikia.

Akizungumza wakati wa tukio hilo lililofanyika Julai 04, 2024 kwenye Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba yanayofanyika kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, Meneja Mauzo na Masoko wa Oryx Gas, Shaban Fundi alisema wameamua kumchagua Shilole kwasababu ni miongoni mwa wadau wanaohamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia.

Naye Shilole alisema yupo tayari kushirikiana na wadau wengine kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan katika kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia.

No comments:

Powered by Blogger.