Bilioni moja zakamilisha ujenzi wa vituo vya afya Mtwara
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com

Huduma mbalimbali za kijamii ikiwemo afya, elimu, maji na utawala bora zinaimarishwa ikiwa ni sehemu ya Uwajibikaji wa Shirika kwa Jamii (CSR).
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa TPDC Marie Msellemu amesema Shirika hilo limetoa jumla ya Bilioni moja ili kuinua sekta ya afya mkoani Mtwara ambapo milioni 600 zimetolewa kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya kijiji cha Msimbati na Tsh milioni 400 zimetolewa kukamilisha ujenzi wa kituo cha afya kijiji cha Nyundo kilichopo Kata ya Nyundo wilaya ya Nanyamba.
Aidha, akiongea na wananchi wa Nanyamba, Mbunge wa Nanyamba Chikota ameishukuru TPDC kwa kuendelea kuunga mkono juhudi za serikali kwenye kuboresha sekta ya afya.
"TPDC amekuwa mdau wetu mkubwa wa maendeleo mkoano Mtwara, tunashukuru uongozi wa TPDC kwa kutupa fedha za kukamilisha kituo cha afya kata ya Nyundo Tsh milioni 400 ambapo kukamilika kwa kituo hiki cha afya tunatarajia kitawapunguzia wananchi gharama za usafiri ili kufuata huduma" alieleza Chikota.
Wananchi wa kijiji cha Nyundo wameishukuru TPDC kwa kutoa fedha za kamilishakutoa ujenzi wa Zahanati hali ambayo itapunguza vifo hasa vya kina mama wajawazito.
No comments: