Wakazi Iringa wakumbushwa usafi na utunzaji mazingira
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Peter Serukamba amewakumbusha wakazi mkoani humo kufanya kweli katika ufanyaji wa usafi wa mazingira.
‘’Hakika sisi watu wa Iringa, hatubaki nyuma, tunaendelea mbele na tutafanya kweli. Pia kufanya usafi ni sehemu ya maisha yetu’’ alisema.
Serukamba alisema katika kuhakikisha hawabaki katika usafi wameunda kamati malumu za kusimamia usafi kuanzia ngazi ya Halmashauri hadi Mkoa.
‘’Tumeunda kamati kuanzia ngazi ya Halmashauri mpaka mkoa na kila baada ya wiki mbili tunakutana mkoani kwajili ya kuja kuripoti kinachoendelea kwenye eneo la usafi kwa kila Halmashauri. Kampeni hii tumeiwekea miundo mbinu ya kusimamia kuhakikisha inatekelezwa’’ alisema.
Kwa upande wake Afisa Utamaduni Mkoa wa Iringa, Steven Sanga alisema kwa upande wa ufanyaji wa mazoezi, mkoa wa umeweka utaratibu malumu wa kufanya kweli kwa kufanya mazoezi kila Jumamosi.
‘’Mkoa wa Iringa, tumekuwa na mazoezi yanayofanyika kila Jumamosi kwa watumishi, wananchi na wafanyakazi wa taasisi mbalimbali’’ alisema.
Sanga alisema mazoezi wanayofanya ni kukimbia pamoja na kutembea ambapo mazoezi huanzia kwa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Iringa mpaka Kihesa-Kilolo.
No comments: