Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Felister Mdemu akizungumza na wanawake wajasiriamali kupitia Jukwaa la Wanawake Wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli za jukwaa hilo iliyofanyika Jumanne Agosti 20, 2024.
Ziara hiyo ni sehemu ya kufuatilia jitihada za Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum katika kuwainua wanawake kiuchumi kupitia afua za Jukwaa la Kizazi Chenye Usawa.
Mdemu amewahimiza wanawake wilayani Kwimba kuendelea kujiunga katika vikundi ili kunufaika na mikopo isiyo na riba inayotolewa na Halmashauri ambapo Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameweka mazingira rafiki na wezeshi ili mikopo hiyo kuwanufaisha wanawake.
Na George Binagi- GB P azzo, BMG
Katibu Tawala Wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza, Mohamed Mtulyakwaku akiwasilisha salamu za Wilaya hiyo kabla ya kumkaribisha Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Felister Mdemu kuzungumza na wanawake wajasiriamali wilayani humo.
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wanawake Wilaya ya Kwimba, Pendo Mchele akieleza manufaa ya jukwaa hilo kwa wanawake na jinsi lilivyowasaidia kujikwamua kiuchumi.
Wanawake wajasiriamali wilayani Kwimba wakimsikiliza Juliana Kibonde ambaye ni Mkurugenzi Msaidizi Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum anayeshughulikia Idara ya Jinsia.
Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Kwimba, Rosalia Magoti akieleza namna mikopo inayotolewa na Halmashauri inavyowasaidia wanawake kujikwamua kiuchumi.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Felister Mdemu akikagua bidhaa mbalimali zinazozalishwa na wanawake wajasiriamali kupitia Jukwaa la Wanawake Wilaya ya Kwimba.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Felister Mdemu akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wilayani Kwimba, na wanachama wa Jukwaa la Wanawake Kwimba.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Felister Mdemu akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wilayani Kwimba, na wanachama wa Jukwaa la Wanawake Kwimba.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Felister Mdemu akiwasili Sumve wilayani Kwimba kukagua vikundi ya wajasiiamali wanawake vya Upendo na Jikomboe vilivyonufaika na mikopo ya asilimia 10 kutoka Halmashauri.
Mwenyekiti wa kikundi cha wanawake cha Upendo, Mary Kalinga akieleza namna walivyojikwamua kiuchumi kupitia mikopo ya Halmashauri.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Felister Mdemu akiwa kwenye picha ya pamoja na wanachama wa kikundi cha Jikomboe.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Felister Mdemu akizungumza na wanawake wajasiriamli kutoka vikundi vya Upendo na Jikomboe vilivyopo Sumve wilayani Kwimba.
Mwenyekiti wa kikundi cha Jikomboe, Leticia Madaha (kushoto) akimlisha keki Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Felister Mdemu (kulia) baada ya kukagua shughuli za kikundi hicho.
No comments: