LIVE STREAM ADS

Header Ads

DC Sengerema azindua tawi la mashabiki wa Pamba Jiji FC

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Mkuu wa Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza, Senyi Ngaga amezindua tawi la mashabiki wa timu ya Pamba Jiji FC ikiwa ni hamasa kuelekea Siku ya Pamba (Pamba Day) itakayofanyika Agosti 10, 2024 CCM Kirumba.

Uzinduzi huo umefika Agosti 05, 2024 mjini Sengerema ukiambatana na zoezi la uuzaji tiketi za Pamba Day ambapo wana Mwanza wamehimizwa kujitokeza kwa wingi siku hiyo ili kushuhudia timu ya Pamba Jiji FC ikicheza na timu ya Vitalo kutoka Burundi.

Mjumbe wa Kamati ya hamasa kuelekea Pamba Day Mohamed Bitegeko amesema zoezi la uuzaji tiketi linaendelea vizuri ambapo hadi sasa zaidi ya tiketi elfu 20 zimeuzwa ambapo lengo ni kuungana uwanja wa CCM Kirumba.
Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Senyi Ngaga akizungumza wakati wa uzinduzi wa tawi la mashabiki wa timu ya Pamba Jiji FC na kuwahamasisha wananchi kununua tiketi.
Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Senyi Ngaga akizungumza wakati wa uzinduzi wa tawi la mashabiki wa timu ya Pamba Jiji FC mjini Sengerema.
Mjumbe wa Kamati ya hamasa kuelekea Pamba Day, Mohamed Bitegeko ambaye pia ni Afisa Michezo Halmashauri ya Jiji la Mwanza akizungumza wakati wa uzinduzi wa tawi la mashabiki wa Pamba Jiji FC mjini Sengerema.
Mjumbe wa Kamati ya hamasa kuelekea Pamba Day, Mohamed Bitegeko ambaye pia ni Afisa Michezo Halmashauri ya Jiji la Mwanza akizungumza wakati wa uzinduzi wa tawi la mashabiki wa Pamba Jiji FC mjini Sengerema.
Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Senyi Ngaga akizindua tawi la mashabiki wa Pamba Jiji FC mjini Sengerema.
Pokea jezi bora kabisa za Pamba Jiji FC

No comments:

Powered by Blogger.