LIVE STREAM ADS

Header Ads

Watanzania tumuunge mkono Rais Samia- CANAL

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Rasi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan anapaswa kutiwa moyo na kuungwa mkono kwa maendeleo makubwa anayoyafanya kwa ajili ya watanzania sio kubezwa au kumkejeli.

Wakati Tanganyika inapata uhuru mwaka 1961 kulikuwa na Chuo Kikuu kimoja ila kwa sasa ambapo ni Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, sekta ya elimu imepaa na kuwa na vyuo vikuu 30 na vyuo vishiriki 12.

Kwenye Wilaya ya Iramba kulikuwa na shule nne za msingi na sasa zipo za msingi 111 ambapo za serikali ni 108 na shule binafsi ni tatu, kwa upande wa shule ya sekondari Wilaya ya Iramba likuwa na shule 1 na sasa zipo 29 ambapo za serikali ni 26 na za binafsi zipo tatu.

Hayo yamebainishwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa WazoHuru Media Group Ltd, Mathias Canal, tarehe 19 Septemba 2024 alipokuwa mgeni rasmi katika mahafali ya 61 ya Shule ya Msingi Kiomboi-Bomani iliyopo Wilayani Iramba katika Mkoa wa Singida na kuongeza kuwa Rais Samia ni mwanasiasa mstahimilivu na mwenye utulivu wa hali ya juu katika uongozi wake.

Mathias alieleza kuwa mwaka 2022 Serikali ilifanya mapitio na Mabadiliko ya mitaala na Sera ya elimu ya mwaka 2014 hatimaye kuwa na toleo jipya la sera ya elimu ya mwaka 2023.

Alisema kwa ujumla katika sera hiyo ya elimu kutakuwa na mambo muhimu ikiwemo Kutoa elimu ujuzi badala ya taaluma pekee, na Elimu ya lazima itakuwa miaka 10 badala ya saba.

Mathias Canal alimpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof Adolf Mkenda kwa kuja na wazo la ujenzi wa vyuo vya Ufundi Stadi (VETA) ambapo Wilaya ya Iramba imepokea Bilioni 1.4 na ujenzi wa VETA unaendelea katika Kijiji cha Salala kata ya Old Kiomboi.

Hali kadhalika alimpongeza Mbunge wa Jimbo la Iramba ambaye ni Waziri wa Fedha, Dkt Mwigulu Mchemba kwa kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa miradi mbalimbali nchini ikiwemo katika jimbo lake ambapo katika kipindi cha miaka minne 2020-2024 Wilaya ya Iramba imepokea Bilioni 6.682 kwa ajili ya sekta ya elimu.

Katika mahafali hayo, Mathias Canal alichangia kiasi cha Shilingi 400,000 kwa ajili ya motisha kwa walimu, mipira 6 na jezi jozi mbili. Mipira mitatu na jezi jozi moja kwa ajili ya mchezo wa mpira wa miguu (Football) na mipira mitatu na jezi jozi moja kwa ajili ya mchezo wa mpira wa pete (Netball).
Mathias Canal
Zawadi
Risala
Wahitimu.
Mkuu wa Shule

No comments:

Powered by Blogger.