Mabula akagua ujenzi wa barabara ya Buhongwa- Kishiri- Igoma
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Mbunge wa Jimbo la Nyamagana mkoani Mwanza, Stanslaus Mabula amekagua ujenzi wa barabara ya Buhongwa- Kishiri- Igoma yenye urefu wa kilomita 14 inayojengwa kwa kiwango cha lami kwa shilingi bilioni 22.7.
Mabula amekagua barabara hiyo Jumatano Septemba 25, 2024 na kumwagiza mkandarasi mmsimamizi kampuni ya Interconsult kumsimamia vyema mkandarasi anayejenga barabara hiyo, kampuni ya ZHONGMEI Engineering Group ya China kukamilisha mradi huo kwa wakati.
"Maombi ya barabara hii yamekuwepo kwa muda mrefu, tunashukuru kwa umakini wa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kufanikisha ujenzi wa barabara hii" alisema Mabula.
Mabula alisema kukamilika kwa barabara hiyo kutafungua fursa za kibiashara katika Jiji la Mwanza na pia kuondoa adha na changamoto kwa wananchi kutumia muda mrefu kuzunguka kutoka Buhingwa- mjini kati hadi Igoma.
Pia Mabula alizungumza na baadhi ya wakazi wa Igoma ambao nyumba zao zinapitiwa na barabara hiyo na kuwasihi kupisha ili mkandarasi aendelee na shughuli na kueleza kuwa hatua hiyo itasaidia ujenzi kuendelea kwa kasi.
Naye Mratibu wa mradi huo ambaye pia ni Mhandisi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Mhandisi Mkelewe Tungaraza ujenzi huo umefikia asilimia 55 na kwamba wanamsimamia kwa ukaribu Mkandarasi ili kuhakikisha kazi inatekelezwa kwa ubora na kumalizika kwa wakati.
"Japo mkandarasi alianza kazi kwa kuchelewa, lakini sasa ameongeza mitambo ya kutosha na kufanya kazi kwa kasi ili kufidia muda uliopotea mwanzoni. Sina shaka kwamba tutamaliza kazi kwa wakati na kwa ubora, na hii ni mara ya kwanza anafanya kazi nchini hivyo anatambua anapaswa kufanya kazi nzuri ili aendelee kupata kazi nyinine" alisema Mhandishi Msimamizi wa mradi huo, Mhandisi Jared Kweba.
Kwa mjibu wa mkataba, ujenzi ulianza Novemba 20, 2024 na unatarajiwa kufikia tamati Februari 19, 2025
Na George Binagi- GB Pazzo, BMG
Ujenzi huu unajumuisha urefu wa Kilomita 11 kutoka Buhongwa, Kishiri hadi Bango na kipande kingine cha Kishiri hadi Igoma chenye urefu wa kilomita tatu na hivyo jumla ya urefu wa mradi kuwa kilomita 14.
Tazama BMG TV hapa chini
PIA>>> BONYEZA HAPA KUSOMA ZAIDI
No comments: