LIVE STREAM ADS

Header Ads

DC Nyamagana ahimiza wananchi kujiandaa na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, Amina Makilagi akizungumza na wawakilishi wa makundi mbalimbali ya kijamii ikiwa ni mwendelezo wa kukutana na makundi ya kijamii ili kuhamasisha wananchi kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa- Novemba 27, 2024.
Wawakilishi kupitia makundi mbalimbali jijini Mwanza wakiwa kwenye mkutano wa kutoa hamasa ya kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaoarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024.
Wananchi wa Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza wametakiwa kushiriki kikamilifu michakato ya uchaguzi ili wawe na sifa ya kuchagua na kuchaguliwa katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024.

Wito huo ulitolewa Oktoba Mosi na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Amina Makilagi wakati akizungumza na mashirika yasiyo ya kiserikali na vikundi mbalimbali vya wajasiriamali katika ukumbi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza ikiwa ni mwendelezo wa kukutana na makundi mbalimbali kwaajili ya kuhamasisha wananchi kushiriki uchaguzi huo.

Makilai alisema zoezi la kujiandikisha kwenye daftari la wakazi kwa ajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa litaanza Oktoba 11 hadi 20 mwaka huu ambapo amewaomba wananchi kujitokeza kwa ajili ya kujiandikisha.

"Nchi yetu tunapaswa tuijenge wote jitokezeni kugombea nafasi mbalimbali ikiwemo uenyekiti wa mtaa kikubwa ni kuwa na sifa, na mnapaswa kutambua kuwa wenyeviti wa mtaa ndio msingi wa maendeleo katika jamii hivyo mnatakiwa kuchagua viongozi bora watakaondeleza mnyororo wa maendeleo" alisema Makilagi.

Kwa upande wake Maida Husseni ambaye ni mjasirimali kutoka kikundi cha 'Tuinuane Group' kilichopo Mtaa wa Mabatini wilayani Nyamagana, alisema atashiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ili aweze kuchagua kiongozi sahihi.

Naye Katibu Mhutasi wa Shirika la 'Immacate Foundation', Kassim Abdul alisema wataendelea kutoa elimu ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa watu wanaowahudumia ili kushiriki uchaguzi huo kikamilifu.

No comments:

Powered by Blogger.