Bilioni 12.7 kunufaisha wataalamu wa afya Tanzania
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Mwendo ni uleule wa kuhakikisha Tanzania inakuwa kitovu cha utaalamu na wataalamu bobezi wa afya.
Na hilo ndilo hitaji la Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ndio maana amekuwa mwepesi wa kukaribisha washirika mbalimbali ili kushirikiana na Tanzania katika kuboresha Sekta ya Afya kuanzia ngazi ya wataalamu, vifaa tiba na miundombinu yake kwa ujumla.
Kiu hii ya Rais Samia imemfanya kuridhia Serikali yake kupitia Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) na Sweden kusaini makubaliano ya ruzuku ya Shilingi bilioni 12 .7 kwa miaka sita ili kuimarisha utafiti, uvumbuzi na mafunzo kwa wanafunzi wa Uzamivu na Shahada ya Kwanza, ambapo utekelezaji wa mkataba huo utaanza rasmi Desemba 2024 na kuendelea hadi Juni 2030.
Katika ushirikiano huo, MUHAS pia inashirikiana na vyuo vikuu vitatu vya Sweden, vikiwemo Chuo Kikuu cha Uppsala na Taasisi ya Karolinska, ambao watashiriki kama wasimamizi wenza wa wanafunzi wa PhD.
Ushirikiano huo umelenga katika kuimarisha jukumu na uwezo wa chuo kikuu kushughulikia changamoto muhimu za kiafya za umuhimu wa kitaifa, kama vile rasilimali watu kwa afya, sera za afya na miongozo na mabadiliko ya mazingira ya magonjwa.
#KaziInaongea
No comments: