LIVE STREAM ADS

Header Ads

Rais Samia: Mwepesi wa kushukuru, kusamehe

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Bado siku mbili kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vitongoji na Vijiji Novemba 27, 2024 tujiandae.

Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kiongozi mnyenyekevu asiye na hinda na ni mwepesi wa kushukuru na kusamehe popote pale.

Hilo amelionesha dhahiri jana mara baada ya Chuo Kikuu Mzembe kumtunuku Shahada ya Udaktari wa Heshima (Honoris Causa) katika uongozi.

Rais Dkt. Samia ameishukuru Seneto ya chuo hicho kwa kutambua mchango wake kwenye uongozi.

"Ninaishukuru Seneti ya Chuo Kikuu Mzumbe mkoani Morogoro kwa kunitunuku Shahada ya Udaktari wa Heshima (Honoris Causa) katika Uongozi kwenye Mahafali yake ya 23"; 

"Ni heshima kubwa sana kwangu kwa Chuo hiki ambacho kilinilea, kunijenga na kunitayarisha, kutambua mchango wangu katika kuliongoza Taifa letu. Ninaitoa Shahada hii kwa wote wenye mchango katika utekelezaji wa wajibu wangu wa kuitumikia nchi yetu pamoja na Watanzania wote" alisema.

Rais Samia alitoa shukurani hizo kwenye mitandao yake ya kijamii kuonyesha kujali, kuthamini na kuheshimu hilo.
#KaziInaongea

No comments:

Powered by Blogger.