Serikali yashughulikia malalamiko ya wagonjwa Ulanga
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Hatua ya Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kukamilisha ujenzi wa kituo cha kupoza umeme cha Ifakara imesaidia kwa kiasi kikubwa kuondoa malalamiko ya wananchi ya kuchelewa kupata huduma za afya kwenye Hospitali ya Wilaya ya Mahenge.
Hayo yamethibitishwa na Katibu wa Afya Hospitali ya Wilaya ya Ulanga, Goodluck Malya ambae amesema kabla ya kuwepo kwa huduma ya nishati kutoka kwenye kituo hicho, hali ilikuwa ni mbaya kwani kuna huduma zilikuwa hazipatikaniki, lakini pia gharama za nishati zilikuwa za juu kutokana na kutumia genereta.
"Toka kuwashwa kwa kituo cha kupoza umeme Ifakara, Hospitali ya wilaya ya Ulanga imeona mabadiliko makubwa, kwa huduma mbalimbali zinazotegemea nishati ya umeme zimekuwa na mafanikio makubwa.
"Awali kuna mambo yalikuwa hayawezi kufanyika na hospitali ilikuwa ikiingia gharama kubwa katika shughuli za uendeshaji hasahasa katika nishati ya umeme, lakini baada ya kukamilika kwa kituo hicho cha kupoza umeme kumekuwa na mabadiliko makubwa.
"Kwa sasa miundombinu na vifaa vya hospitali vinavyohitaji umeme, vimekuwa vikitumika bila hofu ya kukatika katika kwa umeme. Hatua hiyo imesaidia kupandisha mapato ya hospitali tofauti na kipindi cha nyuma, lakini pia malalamiko ya wananchi juu ya kukosa au kuchekeweshea huduma yamepungua sana."
Serikali ya Rais Samia kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa kushirikiana na Umoja wa Ulaya (EU) wamewezesha ujenzi wa kituo hicho ambacho kimeongeza upatikanaji wa umeme wa uhakika katika Wilaya za Ulanga, Malinyi na Ifakara.
Haja ya mja hunenwa, uungwana ni vitendo. Moja ya ahadi za Rais Samia ni pamoja na kuhakikisha anamaliza changamoto za umeme nchini na vijiji vyote vinafikiwa na huduma hiyo muhimu.
#KAZIINAONGEA
No comments: