Jitihada za kuzuia upotevu wa umeme zaendelea
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Serikali ya wamu ya sita, inaendelea kupambana kuhakikisha kila Mtanzania anapata huduma bora ya Nishati ya Umeme sambamba na kupata elimu ya matumizi bora na sahihi ya nishati hiyo ikiwa ni pamoja na kulinda upotevu wa umeme nchini.
Katika kutekeleza mkakati huo, Serikali chini ya Uongozi wa Rais. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kupitia Wizara ya Nishati, imekuwa ikifanya mikutano kwa kuwashirikisha wadau mbalimbali, kwa lengo la kutoa elimu ya jinsi ya kupunguza matumizi ya umeme pamoja na kutumia vizuri Nishati hiyo inayopatikana nchini.
Kwa mwaka huu wa 2024, Serikali kupitia Wizara ya Nishati, imejiandaa kushiriki katika Mkutano Wadau wa matumizi bora ya Nishati, Mkutano Mkuu wa Kikanda (REEC20204) Jijini Arusha Desemba 4-5, 2024.
Naibu Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko, amesema kuwa, Mkutano huo utahusisha nchi zote za SADC pamoja na baadhi ya nchi nyingine Barani Afrika ambapo wadau mbalimbali wanatakiwa kushiriki katika mkutano huo.
Mkutano huu mkubwa utafadhiliwa na Jumuiya ya Umoja wa Ulaya (EU) na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), una lengo la kuhamasisha matumizi bora ya Nishati ambapo kiasi kikubwa cha umeme unaopotea hapa nchini ni kikubwa kati ya asilimia 14.
Mkutano huu unalengo la kuelemishana juu ya utunzaji umeme unaopotea na matumizi bora ya Nishati ya Umeme na umeme unaopotea uweze kutosheleza na hii ni fursa pekee ya kuweza kujifunza utunzani wa umeme.
Mwaka 2023 Wizara ya Nishati, Umoja wa Ulaya pamoja na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), walianza majaribio ya mradi wa matumizi bora ya Nishati kwa kuzijengea uwezo wa namna ya kufanya tathmini ya matumizi ya Nishati na kudhibiti matumizi ya umeme kwa Taasisi na Viwanda nchini na tayari mradi huo unatekelezwa kwa gharama ya Shilingi Bilioni 24.18 (Euro Milioni 19).
#KAZIINAONGEA
No comments: