Rais Samia awaahidi makubwa wafanyabishara wa utalii
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Ni mtu wa watu, anapendwa na anakubalika na watu wa rika na kada mbalimbali na ndio maana hata wafanyabiashara wa utalii wa Arusha na Kilimanjaro hawakuona udhia kutoa magari yao zaidi ya 500 kwa ajili ya kwenda kumpokea mama, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Upendo huo uliooneshwa na wafanyabiashara wa utalii kwake ulimfanya Rais Samia kuwaahidi mambo makubwa wafanyabiashara hao.
Msafara mrefu wa magari ya kitalii zaidi ya 500 ulikwenda kumpokea Rais Samia kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).
Mara baada ya kutua, Rais Samia aliwashukuru Wafanyabiashara na wadau wa utalii waliofika kumpokea na kusema kuwa suala hilo limekuwa la heshima kubwa kwake na linampa moyo na ari zaidi ya kuwatumikia watanzania, akiahidi kurudi Mkoani Arusha kwa ajili ya kuzungumza na wafanyabiashara na wadau hao wa utalii.
#KAZIINAONGEA
No comments: