LIVE STREAM ADS

Header Ads

Rais Samia afurahishwa na wananchi wa Arusha

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa pongezi kwa wakazi wa Mkoa wa Arusha, viongozi wa dini na wadau wa Utalii kwa kuendelea kutunza amani na utulivu.

Rais Samia amesema hatua hiyo imechangia ongezeko kubwa la idadi ya watalii pamoja na mikutano mbalimbali ya kitaifa na kimataifa.

Ametoa pongezi hizo Novemba 27, 2024 alipokuwa akizungumza na Wakazi wa Mkoa wa Arusha, waliofika kumlaki kwenye Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro KIA, Akielekea Mkoani Arusha kwenye ziara ya Kikazi ya siku nne.

Akiwashukuru mamia ya wafanyabiashara na wadau wa utalii waliofika kumpokea na magari ya kitalii zaidi ya 500, Rais Samia amesema suala hilo limekuwa la heshima kubwa kwake na linampa moyo na ari zaidi ya kuwatumikia watanzania, akiahidi kurudi Mkoani Arusha kwa ajili ya kuzungumza na wafanyabiashara na wadau hao wa utalii.
#KAZIINAONGEA

No comments:

Powered by Blogger.