LIVE STREAM ADS

Header Ads

Serikali ya Rais Samia yawahimiza wananchi kupiga kura Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vitongoji na Vijiji

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Sababu 10 kwa nini Tanzania ni eneo salama kuwekeza.


Zoezi la upigaji kura ni la muda mfupi, ambalo halichukui hata dakika 20 kulikamilisha, lakini lina maana kubwa kwa mwananchi kwani linabeba mustakabali wa miaka mitano ijayo.

Kulidharau zoezi hilo kuna madhara makubwa kuliko kuliheshimu, uamuzi mbaya wa sasa unabeba maumivu ya miaka mitano na uamuzi sahihi una faida kubwa kwa kipindi hicho hicho cha miaka mitano.

Hii maana yake ni busara kwa kila mwananchi mwenye sifa ya kupiga kura, kuhakikisha anafanya hivyo ili kuepuka kuutesa mtaa wake, kwani kura moja ina thamani kubwa kwa Mtaa, Kijiji au Kitongoji.

Na hapo ndipo Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia kwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko amewahimiza Watanzania kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 27, 2024.

Dkt. Biteko ametoa rai hiyo Novemba 25,2024 akiwa mkoani Geita ambapo amesema uchaguzi huo ni muhimu hususan kwa ukuzaji wa demokrasia nchini.

“Naomba Watanzania wote waliojiandikisha kwenye Daftari la Kupiga Kura katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika maeneo yao wajitokeze kupiga kura kwa ajili ya kuchagua viongozi wao” amesema Dkt. Biteko.

Amesisitiza “Viongozi hawa ndio msingi katika nchi yetu, viongozi hawa ndio wanajua watu wanaishije, wana shida gani na watafanya nini kutatua shida hizo. Ni muhimu wote kushiriki kuchagua viongozi tunaowataka” amesisitiza.

Aidha Dkt. Biteko amebainisha kuwa kupiga kura ni haki ya kila Mtanzania mwenye sifa hivyo watu wote wenye sifa wajitokeze kupiga kura ifikapo Novemba 27, 2024.
#KaziInaongea

No comments:

Powered by Blogger.