Serikali ya Rais Samia kuanzisha programu mpya ya lishe
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com

Mchakato huu wa Serikali umekuja kufuatia kuibuka kwa hoja kutoka kwa Mbunge wa Viti Maalumu, Dkt. Alice Karungi Kaijage aliyehoji kama kuna haja ya Serikali kuhuisha Taasisi ya Lishe badala ya kuifuta kabisa.
Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel ameeleza Bungeni kuwa, Wizara ya Afya inatarajia kuanzisha Programu ya Taifa ya Lishe pamoja na kuanzisha Kitengo cha Utafiti wa Lishe katika Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR).
Kutokana na kuanzishwa kwa programuhiyo, Seriakali imeona kuna haja ya majukumu yote yaliyokuwa yanatekelezwa na TFNC kufanywa kwa upana wake na Programu ya Taifa ya Lishe.
Tamko la kufutwa kwa TFNC lilitolewa na Msajili wa Hazina Desemba 15, 2023 na kwamba majukumu yaliyokuwa yakitekelezwa na taasisi hiyo sasa yatahamishiwa kwenye Programu ya Taifa ya Lishe pamoja na kitengo kipya cha utafiti wa lishe ndani ya Taasisi ya NIMR.
Hatua za awali za kuanzisha programu hiyo tayari zimeanza, hatua inayolenga kuboresha masuala ya lishe na utafiti wa kisayansi nchini.
#KaziInaongea
No comments: